ZIDANE MENEJA MPYA MADRID
Rafael Benitez
Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtimua kocha wake Rafael Benitez ambaye ana Miezi 7 tu katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu, na nafasi yake imechukuliwa na mchezaji mkongwe mfaransa Zinedine Zidane zizou ambaye awali alikuwa Kocha wa Kikosi B cha timu hiyo .
Hii inatokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka Sare 2-2 na Valencia katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.
Tangu atue Madrid Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona , Pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.
Real ilitoka Sare 2-2 na Kikosi cha Gary Neville, Mchezaji wa zamani wa Man United ambae sasa anaifundisha Valencia, iliyotoka 2-2 na Real Uwanjani Mestalla katika Mechi ya La Liga, Sare ambayo imewaacha Vigogo hao Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid.
Tangu atue Real, Benitez amekuwa si kipenzi cha Mashabiki wa Klabu hiyo, na kutandikwa 4-0 kwenye El Clasico Mwezi Novemba na Mahasimu wao Barcelona hakukumsaidia hata kidogo.
Pia kutupwa nje ya Copa del Rey baada ya kumchezesha Mchezaji asiestahili katika Mechi na Cadiz kumechochea chuki dhidi yake.
Hali hiyo imefanya kuwepo minong’ono ya kila mara kuwa Wachezaji wa Real hawana raha na Benitez na wana mgomo baridi dhidi yake.
Wiki iliyopita Benitez aliwatuhumu Wanahabari kwa kuendesha kampeni kumpinga yeye, Klabu na Rais wao Florentino Peréz.
Comments
Post a Comment