BOMOABOMOA YASITISHWA DAR ES SALAAM

1
Mawakili wa upande wa serikali na walalamikaji wakiandaa nakala zao kabla ya madai hayo kusikilizwa.
2
Wakazi wa Kinondoni wakipongezana baada ya kupokea taarifa za kusitishwa kwa bomoabomoa kwenye makazi yao.
3
Askari wakidumisha usalama.
MAHAKAMA ya Ardhi jijini Dar imesimamisha zoezi la bomoabomoa iliyowakumba wakazi maeneo ya mabondeni wa Wilaya ya Kinondoni baada ya wakazi hao kufikisha ombi hilo mahakamani hapo mapema wiki iliyopita.
Ombi hilo lilitokana na malalamiko ya wakazi wengi walioiomba mahakama izuie bomoabomoa hiyo kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki zao ambapo wengi wa walalamikaji hao walidai kufidiwa kabla ya kuondoka.
Hata hivyo uamuzi huo wa mahakama umewagusa walalamikaji 674 tu ambao wametajwa kwenye malalamiko huku zoezi la bomoabomoa likiendelea kama kawaida kwa nyumba zingine ambazo hazihusiki na kesi hiyo.
Picha: Chande Abdallah/GPL(P.T)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA