FAMILIA UCHINA ZARUHUSIWA WATOTO WAWILI

Sera

Sera ya kuruhusu mtoto mmoja pekee katika familia ilianza kutekelezwa 1978
Familia nchini Uchina sasa zimeruhusiwa kupata watoto wawili baada ya kuanza kutekelezwa kwa sera mpya kuhusu upangaji uzazi.
Sera hiyo mpya imeanza kutekelezwa Ijumaa na kufikisha kikomo sera tata ya awali ambayo iliwaruhusu wanandoa kupata mtoto mmoja pekee.
Sera hiyo imesababisha kuwepo kwa sehemu kubwa ya raia ambao ni wazee na kupungua kwa watu ambao wanaweza kufanya kazi.
Sera hiyo ya watoto waili ilitangazwa Oktoba na chama tawala cha Kikomunisti na kuidhinishwa na bunge la taifa baadaye Desemba.
"Ni vyema kuzingatia jinsi maisha yataathirika,” shirika la habari la serikali la Xinhua limesema.
Sera ya kuruhusu mtoto mmoja pekee katika familia ilianza kutekelezwa mwaka 1978.
Raia Uchina kuruhusiwa kuzaa watoto wawili
Waliopata watoto zaidi waliadhibiwa vikali na hata wengine kulazimishwa kutoa mimba.
Sera hiyo ilizuia kuzaliwa kwa watu 400 milioni.
China
Wanandoa waliojifungua mtoto zaidi ya mmoja waliadhibiwa vikali awali
Idadi ya watu Uchina kufikia 2013 wakati wa kufanywa kwa sensa ilikuwa imefikia 1.357 bilioni.
Kufikia 2050, Uchina inatarajiwa kuwa na watu karibu 500 milioni waliozidi umri wa miaka 60, idadi inayozidi raia wa Marekani.
Utafiti uliofanywa majuzi unaonyesha kwamba licha ya serikali kulegeza sheria ya kujifungua watoto, hakuna msisimko miongoni mwa wanandoa 100 milioni ambao wanaweza kupata watoto wa ziada.
Hii sana inatokana na gharama ya kuwalea watoto

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA