CAMEROON YAAGA WORLD CUP 2010
Cameroon Team
Dalili kwamba mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yanayoendelea huko Afrika Kusini yanaweza kuwa machungu kupita yote kwa bara la Afrika yanaweza kuwa yameanza rasmi kuonekana jana baada ya timu ya Taifa ya Cameroon,maarufu kama Indomitable Lions(Simba wasiofugika) kuwa timu ya kwanza kutolewa katika mashindano hayo.
Cameroon,timu ambayo ilikuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikitajwa kama “tumaini la Afrika”,imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa jumla ya magoli 2-1 na Denmark.
Kwa maana hiyo kutoka kundi E,Uholanzi imejihakikishia kuendelea na mashindano(Best 16) huku Japan ikisubiri kuumana na Denmark katika mchezo ambao utaamua nani aendelee na nani atoke.Kutoka katika kila kundi timu mbili tu ndizo zinazoendelea.
Comments
Post a Comment