GHANA YAIBEBA AFRIKA


Ghanaian fans

Ghana imefanikiwa kuyabakisha matumaini ya Afrika kulibakiza kombe barani Afrika kwa kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano ya timu 16.

Ingawa Ghana ilibamizwa 1-0 na Ujerumani kwenye uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg, ushindi wa Australia wa mabao 2-1 dhidi ya Serbia uliifanya Ghana isonge mbele kwa tofauti ya magoli.

Ghana imemaliza mechi zake tatu ikishika nafasi ya pili kwenye kundi D na sasa itapambana na mshindi wa kwanza wa kundi A, Marekani siku ya jumamosi.

Akiongea baada ya mechi kocha wa Ghana, Milovan Rajevac alielezea kufurahishwa kwake na jinsi Waafrika Kusini walivyoishangilia kwa nguvu Ghana.

"Tunatumaini Waafrika Kusini wataendelea kutushangilia kwenye mechi zijazo", alisema kocha huyo wa Ghana.

Wawakilishi wengine wa Afrika, Algeria walishindwa kulilinda lango lao dakika za majeruhi na kuwaruhusu Marekani kupata goli la ushindi ambalo limeifanya Algeria irudi nyumbani huku ikishika mkia kwenye kundi C.

Goli la ushindi la Marekani lilifungwa na Landon Donovan kwenye dakika ya 90. Kwa ushindi wake dhidi ya Algeria, Marekani imemaliza mechi zake ikiwa vinara wa kundi C huku Uingereza ambayo iliifunga Slovenia 1-0 ikishika nafasi ya pili.

Marekani itacheza na Ghana jumamosi wakati Uingereza itapimana ubavu na Ujerumani siku ya jumapili.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA