KISWAHILI CHAZIDI KUSHIKA KASI MPAKA MTONI


Nas Damian Marley: Watupia Kiswahili kwenye ngoma yao
Katika kile kinachoonesha kwamba Lugha yetu ya Taifa a.k.a Kiswahili inaendelea kupasua anga ulimwenguni, mastaa wawili wa muziki wa Hip Hop Marekani, Nas Escoba na mtoto wa Hayati Bob Marley, Damian Marley wameitupia lugha hiyo kwenye ngoma yao yenye jina la As We Enter.

Washkaji hao ambao wamesimama vyema kwenye kolabo hiyo ya ukweli ambayo wameimba kwa kupokezana wametumia maneno ya kiswahili kama “Habari gani”, “Nzuri sana” na kuifanya lugha yetu kutambulika na mataifa mbalimbali duniani. Zaidi icheki ngoma hiyo hapo pembeni huku maneno ya kiswahili yakiwa yamewekewa mishale.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA