Club Maisha kufunguliwa upya kesho


mwonekano wa nje wa maisha club




dancing floor inavyoonekana



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Club Maisha kufunguliwa upya

* Ni baada ya kufanyiwa ujenzi

UKUMBI maarufu wa starehe wa Club Maisha unatarajiwa kufunguliwa upya Juni 24 mwaka huu, baada ya kufanyiwa ujenzi mkubwa kutokana na kuungua moto mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey), alisema klabu hiyo imefanyiwa ubunifu mkubwa ili kukonga nyoyo kwa kutoa burudani murua na ya uhakika kwa wateja wake.

“Club Maisha inakuja katika mtazamo mpya kwa kutoa burudani za usiku Dar es Salaam iliyopambwa vizuri, sauti ya kutosha na inaipeleka Tanzania mbele katika kutoa burudani za usiku.

“Baada ya miezi kadhaa wateja wetu kukosa burudani, klabu yao sasa inarudi ikiwa ni ya kisasa zaidi yenye televisheni 32 zitakazokuwa zikionesha fainali za Kombe la Dunia na video za muziki, sehemu mbili za kuchezea, vyumba viwili maalumu vya VIP, hii yote ni katika kuuweka kuwa ya kisasa,” alisema Majey.

Vitu vingine vilivyopo katika Club Maisha ni pamoja na sehemu za kuvutia sigara, varanda ya juu, sehemu saba (7) za baa, jiko na TV kubwa inayoonesha fainali za Kombe la Dunia na michezo mingine kwa nje.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema siku itakayofunguliwa Club Maisha itakolezwa na kusisimuliwa na baadhi ya wachezeshaji muziki (ma-DJ) kutoka Afrika Mashariki na Marekani ambao watapiga nyimbo kali zinazotesa kwa sasa duniani.

“Klabu tayari imekaguliwa na mainjinia kutoka Idara ya Zimamoto pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kuhakikisha hakuna ajali ya moto inayoweza kutokea tena, na milango ya dharura imeongezwa ili kuhakikisha usalama mkubwa unakuwepo,” alisema Majey.

“Tumewekeza vya kutosha ili kuirejesha Club Maisha katika nafasi yake ya ubora kwa klabu za usiku Tanzani, tumeweka staili za kisasa kwa lengo la kutoa burudani iliyotakata kwa wapenda burudani za usiku,” alisema.

Viingilio vitabaki kuwa vya kawaida ambavyo ni sh. 10,000 sehemu ya kawaida na sh. 20,000 kwa VIP.

Ukumbi wa Club Maisha ulifungwa mwaka jana baada ya kuungua moto.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA