Zikiwa zimebaki takribani masaa matano kabla ya tuzo hizi kubwa duniani za BET kuanza kutolewa rasmi, kuna jambo kubwa la kustusha ambalo limewaacha mashabiki wa muziki na maswali mengi ya sintofahamu na kukosa majibu hasa ni jambo gani lililopelekea mpaka tuzo hizi kutolewa kinyemela kwa msanii anayefanya vizuri katika bara la Afrika. Katika kipengele cha Best African Act ambapo kinawakutanisha wasanii wakubwa kutoka bara la Afrika wakiwakilishwa na wasanii kama Mafikizolo (Afrika kusini), Diamond Platnumz (Tanzania), Davido na Tiwa savage wote kutoka Nigeria na Sarkodie (Ghana). Tukio lililotokea nalichukulia kama dharau na ubaguzi wa wasanii wa bara la Afrika,BET wameshindwa kuonyesha dhamani ya wasanii wa Afrika katika tuzo hizo, kabla tukio zima la kuanza kutoa tuzo rasmi kwa washindi wote, msanii Davido amepokelea tuzo yake katika kipengele cha Best African Act aliyoshinda akiwa backstage. Baada ya tuzo davido amewashukuru mashabiki wake kupitia twitte...