HIVI UNAJUA DIAMOND PLATNUMZ AMEJIFUNZIA NYIMBO ZA TAARABU KUIMBA.

Nasib Abdul  aka Diamond Platnumz ana historia yake ya kipekee katika muziki wa kizazi kipya, kama ulikuwa haujui  Diamond Platnumz ashatumia nyimbo za taarab kama za Mzee Yusufu na Marehemu Omary Kopa katika kufanyia mazoezi ya kuimba ili aweze kufikia uwezo mkubwa wa sauti kama ya Mzee Yusuf na Omary Kopa. Diamond amefunguka kupitia kipindi cha leo tena cha Clouds Fm na kutoa acapella za nyimbo za mzee Yusuph na kuzimudu kuziimba vizuri.

Mkali huyo na hitmaker wa "my number One" alivunja record ya aina yake katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards kwa kuzoa tuzo 7 kwa mpigo na kuvunja record iliyokuwa ikishikiliwa na mkali 20 percent.

Diamond anaondoka nchini kesho kuelekea Marekani katika tuzo za BET  zitakazofanyika Jumapili hii tarehe 29/06/2014 itakayokuwa hosted na Chris Rock akiwa kama nominated katika category ya Best International Act: Africa, ambapo anakutana na wakali wengine kutoka Africa kama Davido (Nigeria),Mafikizolo (South Africa,Sarkodie (Ghana),Tiwa Savage (Nigeria),Toofan (Togo)

.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA