Posts
Showing posts from May, 2016
UTURUKI YASEMA IMEUUA WATU 100 WA IS
- Get link
- X
- Other Apps
Jeshi la Uturuki linasema kuwa mizinga yake imewaua wapiganaji zaidi ya mia moja wa IS nchini Syria. Waturuki wanasema waliwalenga wapiganaji hao, ambao walikuwa wanakaribia kurusha makombora kushambulia Uturuki, upande wa pili wa mpaka, hapo jana. Lakini haijulikani vipi jeshi la Uturuki, liliweza kuhisabi idadi hasa ya hasara iliyosababisha, katika eneo linalodhi-bitiwa na IS, na hakuna njia ya kuripoti kutoka eneo hilo.
Maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa baada ya kusafiri kwa mabasi yaendayo haraka
- Get link
- X
- Other Apps
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI *Ataka watu walipe tiketi rasmi, wafuate taratibu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye mabasi ya mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea. Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa kutumia usafiri huo. Waziri Mkuu alipanda basi hilo saa 3:30 asubuhi na lilianza safari saa 3:33 baada ya kusubiri wengine wapande. Kwa wastani ililtumia kati ya dakika mbili hadi tatu kutoka kituo kimoja hadi kingine. Basi hilo liliwasili Kimara
SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA WA COMORO
- Get link
- X
- Other Apps
Makamo wa Rais wa Muungano wa Comoro Mhe,Jafar Ahmada Sais wa kisiwa cha Ngazija akiapishwa jana na Jaji wa mahakama ya katiba ya Nchi hiyo Mhe,Loutfi Soulaimane (hayupo pichani ) wakati wa sherehe za kuapishwa Rais kanali Azali na makamo wake 3 iliyofanyika jana baada ya ushindi wa uchaguzi Mkuu uliofanyika Aprili 10 na marudio ya uchaguzi huo uliofanyika mwezi mei 11 mwaka huu,hafla ilifanyika uwanja wa mpira mjini Ngazija jana,[Picha na Ikulu.] 26 mey 2016. Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri akitoa hutuba yake katika sherehe za kuapishwa zilizofanyika jana kufuatia kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika April Kumi (10) na uchaguzi wa marudio uliofanyika mey 11 mwaka huu,hafla ya sherehe ilifanyika uwanja wa mpira Mjini Ngazija nchini Comoro, Rais Mstaafu wa Muungano wa Comoro Mhe,Dkt.Ikililou Dhoinine (kulia) akiwa na Rais Mpya wa Muungano wa Comoro Mhe, Kanali Azali Assoumani Boinakheri (wa pili kulia) mara baada ya kuapishwa akiwa