Jela miaka 30 kwa yeyote atakayemhusisha mtoto kwenye dawa za kulevya


SERIKALI imesema kuwa mtu yeyote atakayekamatwa kwa kosa la husisha au kushawishi mtoto kujiingiza katika matumizi au biashara ya dawa za kulevya atahukumiwa kifungo cha miaka isiyopungua 30.

Hayo yamesema na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa Tume ya kuratibu na kudhibiti wa Dawa za Kulevya, Amani Msami kupitia Taarifa ya tume hiyo kwa vyombo vya habari.
Msami alisema adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015 tofauti na Sheria ya Kuzuian Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya Na. 9 ya mwaka 1995 iliyokuwa na mapungufu.

Alisema mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo mpya imeweka adhabu ya kifungo cha maisha na faini ya shilingi Milioni 200 kwa kumiliki mitambo ya kutengeneza dawa za kulevya.

Msami aliongeza kuwa Sheria hiyo pia imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya.

“Aidha, sheria hii imeweka adhabu kali ya kifungo cha maisha pamoja na faini isiyopungua Shilingi Bilioni moja kwa watu wanaofadhili biashara ya Dawa za Kulevya ambao mara nyingi ni watu wenye uwezo,”alisema Msami.

Mkuu huyo wa Kitengo, alisema Serikali kupitia vyombo vya Dola iliwabaini, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa wa dawa za kulevya.

Aliwataja baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa dawa hizo waliokamatwa na kuchukuliwa hatua kuwa ni Ali Khatibu haji (maarufu kwa jina la Shkuba, Mohammed Mwarami (maarufu kwa jina la Chonji na Mwanaidi Mfundo (maarufu kwa jina la Mama Leila).

Msami alisisitiza wito wa Serikali kwa wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kutoa taarifa kuhusu watu wanaojihusisha na biashara ya dawa ya kulevya ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
AddThis Sharing Buttons

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA