Watunukiwa vyeti vya kuhitimu Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu TANAPA


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi (kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuelekea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya waajiriwa wa shirika hilo .


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu.




Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi.




Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi 


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori ,Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu,Raphael Muhuga,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi,Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori,Ndugu Karamaga.


Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa haraka wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi 





Askari wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi. 


Baaadhi ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu. 


Askari wa Hifadhi akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga shabaha wakati wa kuhitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi


Baadhi ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.


Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .


Mhifadhi Sekela Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.


Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori, Martin Loibooki akizungumza wakati wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .


Baadhi ya Wahitimu.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa .


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.


Katibu Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.


Baadhi ya Askari Waliohitimu.






Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani Katavi.
  • Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Katavi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA