Wabongo bana! Washushwa kinguvu kwenye mabasi ya DART kwa kuamua kuzurura nayo


Usafiri wa mabasi yaendayo haraka jana uliwachanganya wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kuchangamkia usafiri wa bure huku wakiibua vituko kutokana na mazoea ya kugombania kupanda, kukaa wawili katika kiti kimoja na kupita njia zisizoruhusiwa. 

Waandishi wetu waliokuwa katika vituo mbalimbali kushuhudia majaribio hayo walishuhudia abiria wengi wakishindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na wahusika ikiwamo wasio na matatizo kuketi kwenye viti vya wenye ulemavu. 

Pia, wapo walioonekana wakizunguka na mabasi hayo kutoka kituo kimoja hadi kingine bila kushuka hadi walipoteremshwa kwa nguvu. 

Juzi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa UDART, Ronald Lwakatare alisema mabasi 140 yangeanza kubeba abiria bure jana na leo katika majaribio. 

Baadhi ya maofisa waliokuwa wakitoa elimu juu ya matumizi ya mabasi hayo, walisema kuna changamoto ya wakazi hao kuelewa haraka mfumo wa malipo. 

Kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa hao, kila abiria atatakiwa kufuata hatua mbalimbali kabla ya kupanda usafiri huo na kushuka. 

Hatua hizo ni kulipa na kupewa kadi ambayo ndiyo itakayotumika kuingia na kutoka katika kituo. Abiria wote wanapaswa kutumia mlango wa mbele au nyuma wakati wa kuingia kwa kugusisha kadi hiyo ambayo ndiyo inayofungua mlango. 

Baada ya kuingia, basi linapofika kituoni, mlango yake hufunguka sambamba na ilipo ile ya kituoni hivyo kutokuwa rahisi kwa mtu yeyote kupenya. Katika utaratibu huo, ni vigumu kwa abiria kuingia na kutoka bila kulipa kutokana na mfumo huo.
  • Imenukuliwa kutoka gazeti MWANANCHI

Comments

  1. I really like your blog.. very nice colors & theme.
    Did you make this website yourself or did you hire someone to do it for you?
    Plz respond as I'm looking to construct my own blog and would like to find out where u
    got this from. many thanks

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA