TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA MATUMIZI YA HUDUMA ZA MITANDAO
Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandishi James Kilaba.
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Tanzania
imepiga hatua kubwa sana katika sekta ya mawasiliano hadi kufikia kuwa
kwenye kundi la nchi zilizoendelea kimawasiliano Duniani.
Takwimu
zinaonyesha kuwa watanzania takribani milioni 39 wana laini za simu za
kiganjani pamoja na watumiaji wa intaneti takribani milioni 20 ambapo
miaka ya nyuma idadi ya laini za simu za kiganjani zilikuwa 2,963,737.
Haya ni
maendeleo makubwa yanayoifanya Tanzania kuwa nchi bora kwa upande wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi
James Kilaba alisikika akisema kwamba,”Ukuaji wa kasi wa sekta ya
mawasiliano nchini umechangia sio tu katika kuboresha maisha ya wananchi
kijamii na kiuchumi bali unachangia sana katika kuinua pato la Taifa”.
Ukuaji huu umetokana na kuwepo kwa sera, sheria, kanuni na mfumo mzuri wa utoaji leseni za huduma za mawasiliano.
Kama wasemavyo wahenga kuwa ya Kaisari tumpe Kaisari basi sifa zote ziwaendee Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kazi nzuri wanazozifanya.
TCRA wana
jukumu la kusimamia shughuli hizo zote wakishirikiana na wadau wa
mawasiliano nchini katika kusimamia na kuzitekeleza kwa makini
sera,sheria na kanuni hizo ili kuwezesha kupatikana kwa huduma za
mawasiliano nchini kote kwa kushawishi uwekezaji ,kusimamia vizuri
ushindani pamoja na kutoa fursa sawa kwa watoa huduma.
TCRA
inaendelea kuhakikisha kuwa rasilimali adimu zikiwemo za masafa na namba
za simu zinatumika kwa makini ili kukidhi mahitaji ya Taifa na
maendeleo ikiwa ni kutekeleza lengo la Serikali la kuwawezesha wananchi
wote kupata habari na kuhakikisha hawaachwi nyuma katika maendeleo ndani
ya karne hii ya utandawazi.
Huduma
hizi za mitandao pia zimegawanyika kutokana na kutofautiana kwa mahitaji
ya wananchi. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, huduma za
mitandao ni kama ifuatavyo; Intaneti, Benki Mtandao, Elimu Mtandao,
Matibabu Mtandao,Biashara Mtandao, Malipo Mtandao pamoja na Mawasiliano
Mtandao.
Huduma
hizi zimekuwa zikirahisisha mambo mengi hasa ya kikazi na ya
kijamii,ukiangalia kwa sasa ofisi zote za umma na za binafsi wanatumia
huduma za mitandao katika kufanya shughuli zao zote za kiofisi kama njia
salama ya kuhifadhi data zao.
Kwa ofisi
za Serikalini wameipa huduma hii jina la Serikali Mtandao
(E-Government) ambapo watumishi wa umma wanashauriwa kutumia mtandao huu
ili kuhakikisha kazi zote za ofisi zinafanyika katika hali ya usalama
na usiri mkubwa.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.
Nuru Mllao anasisitiza umuhimu wa watumishi wa Umma kupata mafunzo ya
huduma za mitandao ili kuepuka matatizo yanayotokana na matumizi mabaya
ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.
“Tumegundua
kwamba watumishi wanahitaji muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao
ya kijamii, hivyo tunashkuru sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa
mafunzo kwa watumishi wetu,”alisema Bi.Nuru wakati wa mafunzo ya
watumishi kuhusu masuala ya mawasiliano.
Kwa
upande mwingine, jamii inatumia huduma za mitandao kwa ajili ya
mawasiliano kupitia intanenti ambapo kama tulivyosema hapo awali jumla
ya wananchi milioni 20 wanatumia huduma za intanenti ambazo zinahusisha
matumizi ya mitandao ya kijamii kama ya facebook, instagramu,WhatsApp,
Forums, Linkedin pamoja na barua pepe katika kuwasiliana kati ya mtu
mmoja na mwingine.
Matumizi
hayo ya mitandao ya kijamii pia ni muhimu kwa wananchi kwa kuwa
inatumika kama njia rahisi katika kupashana habari kwa haraka na kufanya
dunia kuonekana kama kijiji kwani watu hupata habari za masafa ya mbali
kwa haraka.
Kama
tunavyojua “Kizuri hakikosi kasoro”, japokua matumizi ya huduma za
mitandao yana faida nyingi lakini kuna baadhi ya madhara hutokea kama
mitandao hiyo ikitumiwa vibaya.
Meneja
Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy anasema kuwa ongezeko la watumiaji wa
huduma za mawasiliano linaenda sambamba na ongezeko la vifaa mbalimbali
vinavyowezesha mawasiliano hayo kufanyika.
“Miongoni
mwa vifaa hivyo ni pamoja na simu za kiganjani,vifaa vya mawasiliano ya
kiganjani (tablets), kompyuta pamoja na modemu, kadri idadi ya watu na
vifaa vya mawasiliano vinavyoongezeka ndivyo matumizi mabaya ya mitandao
yanazidi kuibuka,”anasema Mungy.
Kuna
baadhi ya wananchi ambao tunaweza kusema hawana maadili ya kutosha ambao
wanatumia vibaya huduma hizi za mitandao kwa ajili ya kujinufaisha kwa
njia zisizo za halali pamoja na kuupotosha umma kwa kutuma vitu ambavyo
viko kinyume na maadili ya mtanzania.
Matumizi
mabaya ya mitandao yanapelekea kuwepo kwa madhara kama ya mauaji, wizi,
ukiukwaji wa maadili, ugomvi na kutokuelewana katika jamii zetu.
Ili
kuzuia madhara haya ni lazima kila mmoja azingatie matumizi sahihi ya
huduma za mitandao. Mamlaka inayosimamia Huduma za Mawasiliano nchini
imeelezea baadhi ya mambo muhimu ambayo yatasaidia kuimarisha usalama
pindi utumiapo huduma hizo.
Unatakiwa
kutotumia nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja
wala kuweka nywila ambazo mambo yako binafsi ambayo yanajulikana kwa
watu wengi ili kuzuia mtu mwingine asipate urahisi wa kubuni kuingia
katika mtandao wa mtu mwingine.
Unashauriwa
kubadilisha nywila mara kwa mara pamoja na kutengeneza nywila ambayo
ina muunganiko wa namba na herufi ili isiwe rahisi mtu mwingine kuibuni
pia nywila ni siri yako hushauriwi kumpa mtu mwingine yoyote.
Aidha,
hutakiwi kuiandika sehemu yoyote kwa ajili ya kumbukumbu wala kukubali
au kujibu barua pepe zinazotoka kwa watu usiowajua kwa kuwa wanaweza
kutumia kama njia ya kufahamu nywila yako.
Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania inawasisitiza wananchi kujifunza njia bora za
kutumia mawasiliano hususani matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ili
iweze kuwanufaisha na kuendelea kukuza uchumi wa nchi kuliko kuitumia
vibaya hatimaye ikaleta madhara ambayo yatasababisha matatizo kwa mtu
binafsi au Taifa kwa ujumla.
Watanzania
tunatakiwa kubadilika kulingana na hali halisi ya maendeleo ya nchi
yetu ambapo kwa sasa teknolojia ya huduma za mitandao inazidi kukua kwa
kasi hivyo kurahisisha zaidi huduma muhimu.
hey there and thank you forr your information – I have certainly picked up something new from
ReplyDeleteright here. I did however expertise several teechnical issues
using this website, sincee I experienced to reload the web site
lots of times previous to I could get it tto load correctly.
I haad been wondering if your web host is OK? Not that I'm complaining,
but slow loading instances times will sometimes affect your
placement in google and could damage your
quality score if ads and marketing with Adwords. Well
I'm adding this RSS to my e-mail and could look out for a lot more
of your respective intriguing content. Ensure that you update this again very
soon.
Goood post. I absolutely apprecate this website.
ReplyDeleteThanks!
Hello jus wanted to give you a quick heads up. The text in your article
ReplyDeleteseem to be running off the screen in Chrome. I'm not sure if this is a format issue
or something to do with web browser compatibility but I figured I'd post to let you know.
The style and design loook great though! Hope you get the problem fixed
soon. Cheers