Wahukumiwa kwenda jela miaka 12 na 27 kwa kughushi nyaraka NHIF


WATU wawili wamehukumiwa kwenda jela kwa makosa ya kughushi nyaraka za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) za kuweza kujipatia dawa katika maduka ya dawa yaliyosajiliwa na mfuko huo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mkazi wa Mahakama ya Ilala, Juma Hassan mahakamani hapo kuwa washitakiwa wote wawili watatumikia kifungo kutokana na makosa yao tisa ambapo mtuhuhumiwa wa kwanza Bakari Ramadhan amehukumiwa miaka 27 jela kwa makosa yote tisa na Ahmed Mohamed amehukumiwa miaka 12 kwenda jela kwa makosa manne.

Washitakiwa hao walibainika Desemba 14, 2014 katika Duka JD Pharmacy lilopo Posta wakiwa wanataka kuchukua dawa na ndipo walikamatwa.

Akizungumzia hukumu hiyo Mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Charles Mjema amesema kuwa wananchi watumie mfumo uliowekwa na NHIF na sio kughushi kutokana na mifumo iliyopo inabaini watu walio halali wa kuchukua dawa.

Amesema kuwa NHIF imeweka utaratibu wa mtu kuweza kupata matibabu na kupata dawa katika mfumo ulio bora kughushi hakuwezi kuwasaidia na akifanikiwa kufanya hivyo jela ina mwita.
  • via Michuzi blog

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA