Posts

Showing posts from November, 2011

RAIS KIKWETE ATIA SAINI MUSWADA WA KATIBA.

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge. Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010. Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo. Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ...

MwanaFA ft Linah - Yalaiti Lyrics

Image
Sshhhh,classic classic.. Keeping the good music alive, That's me job, You my sunshine my moonlight and everything I dream about, Linah,let's go.. Chorus.. Yalaiti,napenda pasi kifani/ Tofauti,sikutilii moyoni/ Sikuachi,leo na kesho peponi/ Anh anh anh anh anh anh I love you/ Verse I Sambaza love kama dawa/ huachi mpaka napagawa/ hata ukisema mi sio Hamis natingisha kichwa/ mapenzi yako yanielemea ka chupa nzima ya tequila/ usirushe somo nakupenda acha masihara/ ina haja gani unishikie fimbo ili nikuskize ka gorilla/ mi ni mtu na mapenzi yangu nishaacha zamani usela/ una matatizo najua,na mi nna yangu boo/ we sit together from this moment,we see them through/ nikikukosea nisute,nipige vibao,nizodoe/ ninunie kwa siku kadhaa ila nnachoomba usinikimbie/ mapenzi ya utemi kwangu hadithi mambo ya kizamani hayo/ ukiniudhi ntapiga kwa khanga ndio nimefunzwa Tanga hivyo/ utaoga mabusu nikufute kwa kumbatio/mpaka kama nikisafiri ukinikumbuka iwe kilio/ sipendi mapenzi napenda mapenzi ...

MANENO KUTOKA KWA PANCHO

Kutoka kwenye wall ya facebook ya producer Pancho Magawa Saymon kasema haya ‎...Ma Fans Latino Nation nielewen Nimesema Sifanyi kazi tena na Joh bt sijasema nina Bifu nae,Sina Bifu na mtu This is True Say ...."Joh Makini what the hell iz that meeeen,Umerekodi ngoma bure credit pia za studio umeshindwa kutoa kwenye Crap Video yako.Um Fed Up Official with You this is Bushit.You pamoja na Huyo Adam juma"

BLACK ON BLACK ALBUM LAUNCH PARTY

Image

KUTOKA SAUT: SHEREHE ZA MAHAFALI YA 13 YAFANA SANA

Image
Wadau wakiwa tayari kwa kutunukiwa shahada zao Ni siku ya furaha kwa kila mhitimu MC wa sherehe hizo za leo Lulu Sanga akiwa kazini kwa kutoa utaratibu katika mahafali hayo. Mwanafunzi bora wa mwaka huu, Joseph Masaba aliyevunja rekodi ya kwa kupata First Class ya 4.7 akipongezwa na mgeni Rasmi Mhashamu baba askofu Jude Thadaeus Ruwa’ichi Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino katika mahafali hayo katika viwanja vya Raila Odinga. Mwanafunzi aliyefanya vizuri kwa upande wa Masters Degree kwa kupata daraja la kwanza la 4.5, Mgisha H. Steven aliyekuwa akisoma shahada ya pili ya sheria akitoka kutoa heshima kwa mgeni rasmi.

MAHAFALI YA PILI YAFANA SANA SIKU YA JANA.

Image
Msafara wa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Benjamni William Mkapa Ukiwa unaingia Kwenye Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma Tayari kwa kuwatunuku Wahitimu hapo jana. Kiongozi Wa timu ya Viongozi Wa Juu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Katika Maandamano ya kuelekea kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo jana. Baadhi ya Viongozi Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiwa Tayari Kwenye Maandamo Kuelekea Kweo kwenye Mahafali ya Pili Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo jana. Viongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiongozwa Na Mkuu Wa Chuo Mh Mkapa Wakiwa wamesimama Wakati Wimbo Wa Taifa unaimbwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma jana. Sehemu ya Wahitimu kama wanavyoonekanawakiwa na furaha baada ya kutunukiwa shahada zao hapo jana. PICHA KWA HISANI YA tzcampusvibe.wordpress.com

HAPPY BIRTHDAY DOGO JANJA

Image

HAPPY BIRTHDAY HISABATI(ADILI MKWELA)

Image
Leo ni birthday ya Adili Mkwela a.k.a "Hisabati",msanii ambaye aliweza kuhit sana na track yake ya "peke yangu"na pia akajiingiza katika utengenezaji wa videoz chini ya Chapakazi. Leo atakinukisha vibaya uwanja wa chuo cha ustawi wa jamii-Kijitonyama akishirikiana na MCs kibao Vinega ndani katika harakati za kukomesha unyonyoji unaoendelea dhidi ya wasanii wa kibongo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA JUMUIA (COMMUNITY DAY)YAFANYIKA CHUO CHA SAUT.

Image
Maadhimisho ya siku ya jumuia (community day)yamefanyika leo hapa chuo cha Mt.Augustino na kuudhuliwa na watu wengi wakiwemo wanafunzi,wahadhili ,wananchi wanaokizunguka chuo pamoja na viongozi wa chuo hiki,maadhimisho yameenda vizuri japokuwa kulitokea tatizo la mvua lakini haikuweza kusimamisha maadhimisho hayo. Dhumuni kuu la maadhimisho ya siku ya jumuia ni wanafunzi kuweza kuonyesha mambo mbalimbali ambayo kila kitivo kinafanya,hivyo inakuwa ni fursa nzuri kwa watu mbalimbali kuweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo walikuwa hawayafahamu yanayofanywa na kila idara chuoni hapa….. Mabanda ambayo yameweza kuvuta umati wa watu ni banda la uhusiano wa umma(Public Relations), Mawasiliano ya Umma (Mass communication),banda la sheria (Law).Baada ya maonyesho hayo wanafunzi wa watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika mlo wa mchana ambao uliandaliwa na chuo. Na hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa maonyesho hayo. Makamu mkuu wa chuo Father Charles Kitima mwenye su...

HOT NEWS.....MADUKA YAVUNJWA IRINGA USIKU WA LEO

Image
Wananchi wakitazama Stationery ya Nyigi iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso ambayo imevunjwa na wezi Mmiliki wa duka la Ferick Urembo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kukuta duka lake limevunjwa na kuibwa mali mbali mbali asubuhi hii. Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakitazama duka la Ferick Urembo ambalo limevunjwa usiku wa leo . Wakati maandalizi ya sikuu kuu za Krismas na mwaka mpya yakianza taratibu ,watu wanaosadikika kuwa ni wezi nao wameanza kufanya maandalizi ya funga mwaka baada ya usiku wa leo kuvunja maduka mawili eneo la Eso katika Manispaa ya Iringa na kuiba mali mbali mbali. Maduka ambayo yamevunja usiku wa leo ni pamoja na duka la Ferick Urembo lililopo eneo la Natioanl katika majengo ya Bakwata , na Nyigu Stationery iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso. Baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamesema kuwa maeneo yao yamekuwa yakilindwa na makampuni ya ulinzi na hadi sasa eneo la tu...

Polisi wazuia maandamano

Image
*Wahofia uvunjifu amani, yalipangwa kufanyika J'mosi *Wanaharakati kutafuta njia nyingine kufikisha ujumbe *IGP Mwema asisitiza jeshi hilo halina nia mbaya SIKU moja baada ya wanaharakati kutoka asasi za kiraia zaidi ya 180, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Jukwaa la Katiba Tanzania kutangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima Novemba 26 mwaka huu, Jeshi la Polisi nchini limeyazuia kutokana na hofu ya kuvunjika kwa amani. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, kwa vyombo vya habari, ilisema kutokana na mchakato unaoendelea wa kupitishwa kwa Muswaada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya nchini, amekuwa akipokea maombi ya kufanya maandamano kutoka taasisi mbalimbali nchi nzima yakiwa na malengo tofauti. Alisema malengo hayo ni pamoja na kupinga muswaada huo na mengine yakiunga mkono jambo linaloashiria kuleta migongano na hatimaye kusababisha uvunjifu wa amani. Alizitaja taasisi zil...

KUTOKA SAUT: SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA ALBINO (UTSS) LAFANYA KONGAMANO LA KUELIMISHA JAMII JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA ALBINO

Image
Shirika lisilo la kiserikali UNDER THE SAME SUN (UTSS) linalojishughulisha na kutetea, kuelimisha jamii juu ya vitendo vya ukatili kwa watu weye ulemavu wa ngozi (ALBINO) leo limefanya kongamano pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino juu ya jinsi gani jamii inaweza kukomesha vitendo vya ukatili kwa Albino hapa nchini. Akizungumza na waandishi wa Habari Mtendaji mkuu wa idara ya habari na uhusiano wa kimataifa wa shirika hilo Mrs. Vicky A. Ntetema alisema kuwa jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana katika kukomesha swala zima la ukatili dhidi ya vitendo vya ukatili kwa walemavu wa ngozi hapa nchini, huku akiitaka serikali kuongeza ulinzi kwa watu wenye ulemavu kwani vitendo vya ukatili vimekuwa vikiripotiwa kila siku kutokea hivyo ni dhahiri usalama wa watu wenye ulemavu wa ngozi ni mdogo. Akizungumzia swala la Waganga wa Kienyeji kama chanzo cha ukatili kwa Albino alisema ” Sioni hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya kufungia leseni zinazotolew...