MwanaFA ft Linah - Yalaiti Lyrics


Sshhhh,classic classic..
Keeping the good music alive,
That's me job,
You my sunshine my moonlight and everything I dream about,
Linah,let's go..

Chorus..
Yalaiti,napenda pasi kifani/
Tofauti,sikutilii moyoni/
Sikuachi,leo na kesho peponi/
Anh anh anh anh anh anh I love you/

Verse I
Sambaza love kama dawa/
huachi mpaka napagawa/
hata ukisema mi sio Hamis natingisha kichwa/
mapenzi yako yanielemea ka chupa nzima ya tequila/
usirushe somo nakupenda acha masihara/
ina haja gani unishikie fimbo ili nikuskize ka gorilla/
mi ni mtu na mapenzi yangu nishaacha zamani usela/
una matatizo najua,na mi nna yangu boo/
we sit together from this moment,we see them through/
nikikukosea nisute,nipige vibao,nizodoe/
ninunie kwa siku kadhaa ila nnachoomba usinikimbie/
mapenzi ya utemi kwangu hadithi mambo ya kizamani hayo/
ukiniudhi ntapiga kwa khanga ndio nimefunzwa Tanga hivyo/
utaoga mabusu nikufute kwa kumbatio/mpaka kama nikisafiri ukinikumbuka iwe kilio/
sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/B...

Chorus..

Verse II
Nshasema sipendi mapenzi napenda mapenzi nawe/
usinikatae utaniumiza mi nna biashara na wewe/
ushaangaliwa niunge tela usingoje mpaka uambiwe/
ushaangukiwa anguka nawe usizubae mpaka irejewe/
kwako ntakuwa Bushoke sitajiuliza ka zezeta/
yetu yawe mahaba mapenzi zamani tumepita/
mi sakafuni we ukingoni mbio zangu haziendi mbali/
una moyo wangu ntapenda bila kujali/hata marefa wana timu zao mama panga matokeo/
pambano lianze najua goli ngapi ngapi leo/
usiache kuvaa nguo ndefu hivi vimini achia vicheche/
mwanamke kwetu staha tunaovipenda sio wote/
akili haziuwezi moyo na wenyewe una ubongo pia/
hauwezi ukafuatafuata kila utakachouambia/
nitajiwapo mapenzi naipata picha yako kwanza/
natamani uipate yangu na iwe inakuliwaza/

Linah..
Toa shaka na wasiwasi moyoni/
Toa shaka na wasiwasi moyoni/
Kukuepuka hilo haliwezekani/
Takushika,leo na kesho peponi/

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA