MASHINDANO YA PRO LIFE YAZIDI KUSHIKA KASI HAPA SAUT


Mashindano ya PRO LIFE hapa chuoni SAUT yamezidi kushika kasi,leo zimechezwa mechi mbili ya kwanza ikiwa ni kati ya Public Relations team (PR) V/S Engineering Team ambapo team ya PR imewalaza Engineering magoli 6-0..hivyo timu ya PR imezidi kuendeleza ubabe wake.
Mara baada ya mchezo wa kwanza kumalizika mechi iliyofuatia ni kati ya timu ya Mass communication v/s vijana wa certificate ambapo Certificate wametoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1 na magoli hayo ya timu ya certificate yamefungwa na Kelvin Kilua ambaye anasoma certicate ya journalism,na Pheremon Kulwa anayesoma certificate ya Accountancy,na goli la mass communication limefungwa na Vincent Kedmund,hivyo vijana wa certificate wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea na mashindano.
Comments
Post a Comment