EPIC NATION YAFANA SANA CCM KIRUMBA

Maelfu ya wakazi wa mwanza waliojitokeza katika tamasha la Epic Nation.
Roma mkatoliki akiwajibika katika stage kuwarusha mashabiki wake waliofurika uwanjani hapo!

Nami nikifatilia show inavyokwenda kwa ukaribu kabisa

Katika Tamasha lililofanyika katika uwanja wa CCM kirumba linalojulikana kama EPIC NATION kupitia mtandao wa ZANTEL Leo limeweza kuwavuta vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza na kuwakutanisha kwa pamoja katika uwanja wa CCM kirumba.kulikuwa na mwaliko wa wasanii kibao kwa ajili ya kuwarusha mashabiki waliofika uwanjani hapo,Wasanii waliopanda jukwaani wameweza kugonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa bongo Fleva uku ROMA akichukua point zote muhimu katika tamasha ilo..kwa kuweza kuwarusha mashabiki wake vilivyo.

Tamasha ili la EPIC NATION lilizinduliwa rasmi jijini Dar Es Salaam likilenga hasa kuwasaidia vijana ambao kipato chao ni cha chini waweze kumudu gharama za kuwasiliana kwa bei nafuu kabisa kupitia mtandao wa ZANTEL, hivyo kwa shilingi Tsh500 tu unapata message 300….kutuma kwenda mtandao wowote,MB 50 kwa ajili ya Internet,dakika 10 za kupiga Zantel kwenda Zantel.

ZANTEL KEEP TALKING.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA