FIFA YAFUTA RASMI UCHAGUZI TFF, YAWAPA ‘LIGHT GREEN’ MALINZI, WAMBURA WAGOMBEE
Rais wa TFF Leodgar Tenga. |
Na Saleh Ally.
Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA)
limetaka kuanzwa upya kwa utaratibu wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF).
Uamuzi huo wa FIFA, maana yake
mchakato huo utaanza upya unawaruhusu wote walioondolewa awali kama Jamal
Malinzi na Michael Wambura kuwa huru kugombea tena.
Malinzi (kulia) |
Pamoja na hivyo FIFA imeitaka TFF
kuanzisha chombo kitakachoitwa kamati ya maadili na hadhi kwa ajili ya
kusimamia mchakato huo.
Awali FIFA ilizuia uchaguzi huo
ambao ulipangwa kufanyika February mwaka huu baada ya kukumbwa ba migogoro,
lakini baada ya kufanya mahojiano na shirikisho hilo, wagombea pamoja na kamati
mbalimbali (FIFA) wametoa maagizo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari
hivi punde, Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema FIFA wamewaeleza kuna kasoro
kati zilizojitokeza huku wakisisitiza kuundwa kwa kamati ya maadili na hadhi
kabla ya Octoba mwaka huu.
Wambura. |
“FIFA wamesema kuwa kuna sehemu
tulikuwa tunakosea, tunatakiwa kuunda kamati ya maadili na hadhi ambayo itakuwa
na mwanasheria ndiyo tuweze kuendesha uchaguzi huu.
“Wamepatupa muda hadi Oktoba na
mchakato wote unaanza upya, wanaotaka watalipia fomu upya na kila kitu kwa sasa
kitakuwa kipya kabisa,” alisema Tenga.
“Kwa kuwa mchakato utaanza mapema, Fifa
wameomba tutengeneze taarifa ya mambo yanavyokwenda kabla ya Octoba ili kuokoa
muda kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.”
Maana yake, Tenga aliyekuwa
amemaliza muda wake zaidi ya miezi mitano iliyopita, ataendelea kuula katika
nafasi hiyo akishughulikia maandalizi ya uchaguzi.
SOURCE: www.gsengo.blogspot.com
Comments
Post a Comment