NAOMBA DUA ZENU WADAU WOTE

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunibariki kila kunapokucha na kuweza kunipa nguvu za kusimama na kufikiri vyema, ndugu zangu sasa wakati unakaribia kabisa wa kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu nayosomea shahada ya mahusiano ya Umma na Masoko.

Zimebaki takribani wiki 8 ambayo ni sawa na miezi 2 hivi kuhitimu elimu hii,jambo lililopo mbele yangu ni hapo kesho katika kutetea utafiti nilioufanya (Research defense) mbele ya jopo la wahadhili, si jambo ndogo waweza kuwa na confidence ya kutosha lakini linapofika swala la Maswali kila mhadhili huwa anauliza kwa jinsi anavyojisikia yeye na pengine hata kukuuliza kitu kisichohusiana na research pia,hivyo nawaomba ndugu zangu basi twendelee kushirikiana katika maombi na kuniombea kwa baba mwenyezi Muumba wa mbingu na dunia niweze kudefend vizuri.

SALA ZENU NI MUHIMU SANA KUFANIKISHA SWALA HILI.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA