KILIO KUANGUKIA JANGWANI AU MSIMBAZI?

Leo ndio leo uwanja wa Taifa wakati miamba miwili ya soka nchini, Yanga na Simba watakapoufunga rasmi msimu wa ligi kuu Tanzania Bara. Yanga ambao tayari wametawazwa kuwa mabingwa wataingia uwanjani huku wakiwa tayari wanajiandaa kwa sherehe rasmi za kukabidhiwa kombe wakati watani wao wa jadi Simba waliovuliwa ubingwa huo watakuwa wakitaka kulinda heshima yao. Katika mchezo uliozikutanisha timu hizi mbili katika mchezo wa kufunga pazia la ligi kuu, Simba ambao walikuwa tayari wametangaza ubingwa walitoa kipigo kikali cha 5-0.

Je unadhani Yanga watalipiza kisasi? Msiba leo utakuwa wapi, Jangwani au Msimbazi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA