KIU YASIMAMISHA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA YA UZAMILI (MASTERS) NA UZAMIVU (PHD)

TAARIFA KWA UMMA
Kampala International University, Dar es Salaam Constituent College (KIU-DCC)
KUSIMAMISHWA KWA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU


Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).


Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;


1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikuwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam


2. KIU ishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapo juu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.
Tume haitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hicho kwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
Angalizo:


Chuo cha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwa mujibu wa Ithibati ya Chuo Husika.


Imetolewa na:
Katibu Mtendaji

source:www.tcu.go.tz
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA