PRECISION AIR YAONGEZA NDEGE MPYA
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk Mwana blog John Bukuku wa www.fullshangwe.blogspot.com akijiandaa kushuka mara baada ya ndege hiyo kurejea Dar es salaam ikitokea Zanzibar jana. Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein ...