WALEMAVU WAFUNGA BARABARA KARUME-ILALA JIJINI DAR

Baadhi ya Walemavu wakijadiliana jambo huku wakisubiri hatma ya mgomo wao kutatuliwa.
UMOJA wa Walemavu Wafanyabiashara Mkoa wa Dar es Salaam (Uwawada),wamefunga barabara ya Uhuru na Kawawa kushinikiza serikali kutoa maelezo kuhusiana na uvunjaji wa meza katika soko la Machinga Complex unaodaiwa kufanywa na askari wa jiji usiku wa jana.
Wafanyabiashara hao wamekaa katikakati ya barabara kwenye makutano ya Barabara ya Uhuru na Kawawa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa na lengo kutaka maelezo ya serikali kuu juu kufanya operesheni usiku bila kufanya ushirikishaji kwa wahusika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kidumuke Kidumuke amesema meza za walemavu zilizopo machinga Compelex ziliwekwa kutokana na makubaliano na kuamuliwa kuweka meza hizo, lakini wamevunja utaratibu waliokubaliana, hivyo kuamua kufunga barabara bila utaratibu.
Kidumuke amesema kutokana uvunajaji huo walemavu baadhi wamepotelewa na mali zao na hakuna mtu ambaye atafidia, hivyo serikali inawajibika kulipa na makubaliano hayo yanatakiwa yawe katika maandishi.
"walemavu tumekuwa tukionewa kutokana na hali zetu lakini leo tunawapa usumbufu wananchi ni kwa ajili ya kutaka haki zetu na tunawataka radhi watusamehe". amesema Kidumuke.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi amesema kuwa kuhusu fidia watafanya uchunguzi ili kuona kama kuna waliopotelewa na mali zao.
Mushi amesema walemavu watarudi katika maeneo hayo na waondoke eneo la barabara ili watu wengine waweze kufanikisha shughuli zao.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA