[video] Mei Mosi 2015: Kauli ya Rais Kikwete kuhusu nyongeza ya mishahara na punguzo la kod

t



Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mei Mosi 2015, ameahidi kuongezeka kima cha chini cha mishahara (kutoka 265,000 hadi kufikia 315,000), ikiwa uchumi utaimarika.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, Rais Kikwete pamoja na mengi aliyoyasema, amewataka waajiri kuendelea kutekeleza sera ya ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi, kulipatia ufumbuzi tatizo la mifuko ya jamii, ushiriki wa wananchi katika kujiandikisha kupiga kura na malipo kwa madeni ya waalimu.

Katika hotuba hiyo Rais Kikwete ameeleza kuwa moja ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani ni kuanzishwa kwa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, ambao utatumika kulipa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini. Amesema mfuko huo utaanza kufanya kazi mwezi ujao na tayari Mkurugenzi wake amekwisha teuliwa.

Kuhusu suala la kima cha chini cha mshahara pamoja na kiwango cha kodi ya mapato katika mishahara, Rais Kikwete amesema kuwa serikali inaendelea kuyafanyia kazi, na huenda katika bajeti ijayo mambo hayo yakawezekana.

Sikiliza sehemu ya hayo yalivyotamkwa kwenye video iliyopachikwa hapo juu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA