Wanafunzi wagoma Vyuo Vikuu Dar es Salaam: Mlimani na St. Joseph


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani wameanza mgomo wa kluingia madarasani kuendelea na masomo na kukufanya mkutano chuoni hapo kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwalipa fedha zao za kujikimu ambazo kwa mujibu wa mkataba zinatakiwa kulipwa wiki ya 8 baada ya kusainiwa kwa mkataba baina yao na serikali lakini mpaka sasa wameingia wiki 11 bila kuwapo malipo hayo.

Wakizungumza na vyombo vya habari katika viwanja vya Chuo hicho, wanafunzi hao wamesema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara na kuwasababishia usumbufu mkubwa wa kulipa madeni yao, ilhali serikali ikiwa inatambua wazi kuwa mtu yeyote hawezi kuishi bila kuwa na pesa ya kujikimu hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam ambao maisha yake yametajwa kuwa juu maradufu.

Wamesema hawana nia ya kufanya fujo za aina yoyote, bali wanachohitaji ni kupata suluhu ya tatizo hilo ambalo limewaathiri kimasomo na kisaokolojia hasa kwa kuzingatia kuwa wengi wao wazazi wanategemea fedha kujikimu za watoto wao kutoka serikalini hatua ambayo imewafanya kutokuwa na bajeti kwa ajili yao hivyo inapofika wakati kama huo wazazi pia huathirika kwa namna moja ama nyingine.

Waziri wa mikopo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shitindi Venance ameeleza kuwa kimsingi matatizo hayo yanatokana na mfumo mbaya wa mamlaka yenye dhamana ya kukusanya fedha za mikopo kwa walioajiriwa, lakini pia serikali yenyewe haijatengeneza mazingira mazuri ya ajira ikiwemo kuwabana wanafunzi hao pindi wanapomaliza masomo yao na kuajiriwa serikalini na hata kwenye sekta binafsi.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya zaidi ya elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi, amesema tayari amezungumza na bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha hizo haraka iwezekanavyo na kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.


Wakati huo huo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Joseph cha Mbezi jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha za kujikimu kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi sasa wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili mazingira ya kupanga nyumba mitaani.

Katika taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao iliyotolewa na makamu mkuu wa chuo cha Mt. Joseph Bw. Loyola Proteep aliyeambatana na Mkuu wa Wanafunzi, "Dean of Students" anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya msingi na kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia madarasani wakati wakifuatilia madai yao kwenye Bodi ya Mikopo bila ya mafanikio na uongozi kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.


  • Taarifa via Channel TEN na ITV

UPDATE/TAARIFA MPYA:

Imeoneshwa cheki kuwa fedha zimeingizwa benki...


  • Nakala imepatikana via WhatsApp

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA