Posts
Showing posts from April, 2010
hizi filamu zetu za kibongo zinajenga?
- Get link
- X
- Other Apps
anti Ezekiel na Steven Kanumba Ki ukweli ukiangalia picha kama hii hapa sidhani kama huko na mzazi wako mkitizama TV utaendelea kutupa macho yako katika TV,jamani wasanii wa filamu tufuate maadili ya kitanzania sometime nashindwa kabisa kuangalia filamu zenu ambazo zimejaa mambo ya mapenzi.....sanaa....kuliko ujumbe mwengine tubadilike tuachane na usasa....tusisahau maadili yetu
IMETIMIA MWAKA MMOJA TANGU MLIPUKO WA MABOMU MBAGALA..
- Get link
- X
- Other Apps
Milipuko ya Mabomu - Mbagala ni tukio lililotokea mnamo saa 11:45 asubuhi ya tar. 29 April ya mwaka wa 2009 katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ni baada ya mabomu kulipuka katika ghala ya silaha ya kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) namba 671 KJ.sasa ni mwaka mmoja tangu yalipotokea.. Mabomu hayo yaliyokuwa yakilipuka kwa mfululizo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 20, kujeruhi zaidi ya watu 200 na mamia kadhaa, wengi wao wakiwa ni watoto, kupotea. Athari nyingine ni uharibifu wa majumba na mali.
TATIZO LA INTANETI LILILOSAMBAA AFRICA,ASIA,EUROP E
- Get link
- X
- Other Apps
Tatizo la intaneti ambalo limelalamikiwa na wenye blogu wengi si tu kuwa limeathiri eneo moja bali limegusa nchi katika mabara matatu - Afrika, Asia na Ulaya. Mmoja wa bloga mashuhuri wa India, Amit Agarwal wa blogu ya labnol.org anaandika na kuthibitisha kupatwa na tatizo hilo na anasema kuwa, tatizo hili limesababishwa na hitilafu katika mawasiliano hayo yaliyopo chini ya bahari na inatarajiwa kuwa yatachukua hadi siku tatu hivi hadi matengenezo yakamilike, "Internet services across India have been affected because of faults in an undersea cable (SEA-ME-WE 4) that carries the majority of Internet traffic between South East Asia and Europe. The repair work is expected to be over in the next 2-3 days.
Amazing technology! Now you can Tarck Flights movemet LIVE online with Casper
- Get link
- X
- Other Apps
I saw another amazing application of technology online today in a website called Casper, I couldn't help it but start to wonder and think of how the world would be like a decade from now. Really amazing stuff! Casper is an innovative web-solution to present aircraft movements in an attractive design, live and recorded traffic is presented using Google Maps. Using a proprietary track processing algorithm really smooth flying aircraft can be shown with speeds up-to 100 times. As I write this post, Casper is displaying LIVE flight movements of planes at the Schipol Int'l Airport in Amsterdam. In this site, you can: - Play-back on different speeds up to 100 times - See different aircraft models for different types - See different coloring of the aircraft depending on height, direction or airline - See the labels near the aircraft with information like call sign, aircraft type, height, speed, etc. - See the trails behind the aircraft Explore more atL casper.frontier.nl
AINA MPYA YA UTAPELI TANDO - Barua yenye mhuri, tarehe na saini!
- Get link
- X
- Other Apps
Kadiri siku zinavyosonga, ndivyo na watu wanavyotumia intaneti na kadiri ya matumizi ya intaneti yanavyoongezeka ndivyo na vitendo vya kidanganyifu na wizi wa mitandaoni vinavyoongezeka. Kujifunza kung'amua mbinu wanazozitumia matapeli katika kufanikisha malengo yao ndicho kiokozi muhimu katika kujilinda wewe binafsi na wale unaowajali dhidi ya upotevu wa fedha na mali. Kwa bahati mbaya, matapeli kama ilivyo kawaida yao, hawakomi kujaribu kuvumbua mbinu mpya za kuiba pale wanapogundua kuwa watu wengi wameshazifahamu na kuzizoea mbinu zao. Siku tatu zilizopita nimepokea ujumbe kama unavyosomeka kwenye picha inayoonekana hapo (bofya kuikuza ili kupata ukubwa unaosomeka kirahisi zaidi) na katika ujumbe huo, hakukuwa na maelezo zaidi ya 'respond to the subject matter'. Nilifungua kiambatanisho hicho na kusoma maelezo hayo. Yafuatayo ni mambo muhimu ya haraka niliyotumia kung'amua kuwa ujumbe huu ni wa kitapeli. 1. Tarehe iliyopo katika mhuri ni 05.05.10, mbona bado hatuj
Nameless kutumbuiza miss universe
- Get link
- X
- Other Apps
AY AND NAMELESS Mwanamuziki kutoka nchini Kenya atambulikae kwa jina la Nameless pichani (kulia) akiwa na msanii Mwenzake wa Tanzania Ambwene Yesaya a.k.a AY muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar leo. Nemeless ni mmoja wa wasanii watako tumbuiza katika shindano la Miss Universe Aprili 23, 2010 katika ukumbi wa Mlimani City.
Miss Universe kutifuana leo
- Get link
- X
- Other Apps
Warembo ishirini kutoka mikoa mbalimbali leo wanaratajiwa kutifuana kwenye shindano la kumtafuta mrithi wa taji la Miss Universe 2010/2011 ambalo mpaka sasa linakamatwa na Illuminata James. Mkurugenzi wa Campass Communication Ltd, Maria Sarungi amesema fainali za kumtafuta mnyange huyo zitafanyika leo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar es Salaam. Maria alisema kuwa kila kitu kimeshakamilika na pambano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na kila mrembo kuwa na vigezo vinavyokubalika. taarifa hii ni kwa hisani ya globalpublishers website
KLABU YA SIMBA YATAMBULISHA TIMU YA SIMBA YA WANAWAKE
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya SIMBA imetambulisha timu yake ya soka kwa wanawake wenye miaka 12 hadi 17 ambapo imewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu wanapokuwa katika michezo mbali mbali. Akizungumza kwenye utambulisho wa timu hiyo katika uwanja wa KARUME, Katibu mkuu wa SIMBA MWINA KADUGUDA amesema kuwa mchezaji akiwa na nidhamu anaweza kuenedelea katika soka kama timu ya SIMBA ilivyo. Timu hiyo inajiandaa kushiriki katika mashindano ya wilaya ya ILALA ya soka la wanawake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kwa upande wake mwanzilishi wa timu hiyo STEPHANIA KABUMBA na kocha wa wachezaji hao ANTONY MAKUNJA wamesema wachezaji hao wanajitahidi kufanya vyema kwenye mazoezi na kudai kuwa watahakikisha timu hiyo inaendelea zaidi ili kupata wachezajiw azuri watakakwenda kwenye timu ya TAIFA ya wanawake
Viongozi kudhibiti zana za Nuklia duniani!
- Get link
- X
- Other Apps
Viongozi wa mataifa makubwa na yenye nguvu duniani katika picha ya pamoja. Viongozi wa zaidi ya nchi arobaini waliohudhuria mkutano kuhusu usalama mjini Washington, Marekani, wamekubaliana kulinda malighafi za nuklia kote duniani na kuhakikisha hazifiki mikononi mwa makundi ya kigaidi. Akifunga rasmi mkutano huo, rais Barack Obama, alisema makubaliano yaliyoafikiwa ni ishara kuwa dunia sasa ni mahala salama. Viongozi hao wamesema katika miaka minne ijayo watahakikisha kuwa vitu vyote vinavyohusiana na nyuklia vinadhibitiwa. Walitilia mkazo umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa katika kukabiliana na silaha hizo na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa nuklia. Mkutano huo pia umetoa makataa ya miaka minne kwa nchi zenye zana hizo kuzidhibiti vyema na kushirikiana kuzuia biashara za zana hizo chanzo cha habari ni http://www.bbcswahili.com/
SHOGA TAABANI JERA YA MALAWI
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito wa kumpatia msaada wa haraka mwanaume mmoja anayehjihusisha na mapenzi ya jinsia, aliye gerezani nchini Malawi anayeelezewa kuumwa sana. Mwanaharakati Peter Tatchell amesema amepokea taarifa kutoka gereza la Chichiri kwamba Steven Monjeza anayeendelea na kesi ya uhusiano wake wa kimapenzi na mwanaume mwenzake, hajatibiwa na amekuwa akitapika na kulalamika maumivu ya kifua kwa zaidi ya siku kumi. Taarifa zaidi zimesema anazuiliwa katika jela yenye msongamano mkubwa na ni chafu. Monjeza na mpenzi wake Tiwonge Chimbalanga, wanashtakiwa kwa kuikuka sheria iliyowekwa nchini Malawi inayopiga marufuku ndo za watu wa jinsia moja . Wapenzi hao walifanya sherehe ya ndoa yao mwezi wa Desemba na wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha mika kumi na minne jela ikiwa watapatikana na hatia.
MARUFUKU KUPIGA MUZIKI RADIONI SOMALIA
- Get link
- X
- Other Apps
Haya tena, huko Somalia stesheni za radio zimepigwa marufuku kurusha matangazo yanayoambatana na muziki. Amri hiyo iliyotolewa na waasi wa kundi la Hizbul-Islam, ambao ni waislamu wenye msimamo mkali, inaanza kufanya kazi mara moja. Kinyume na utekelezaji wa amri hiyo, vituo na watangazaji wa radio watakuwa katika hatari ya kupoteza maisha yao. Mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Mogadishu amesema amri hiyo inafanana sana na ile ya Taliban ya kule Afghanistan.
MWANAFUNZI WA KIKE AUWAWA KIKATILI GESTI
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Sara Nguzo, aliyekuwa akiishi Kigogo Mbuyuni, Dar es Salaam, amekutwa ameuawa chumba namba 9 cha nyumba ya kulala wageni iitwayo Makambe, iliyopo Ilala Mchikichini jijini. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia Aprili 5, mwaka huu ambapo uchunguzi wetu unaonesha Mwanafunzi huyo alifika katika gesti hiyo na kijana mmoja na kuchukua chumba kwaajili ya kujipumzisha. Wandishi wetu walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kumhoji mhudumu aliyejitambulisha kwa jina la Pricila Shirima, ambaye ndiye aliyewapa chumba alisema; “Mwanafunzi huyo alifika kwenye gesti hiyo na mwanaume ‘Fataki’ mmoja mrefu, mweusi aliyevaa kofia nyeusi na kaptula, majira ya saa mbili usiku. “Walipofika waliomba niwapatie chumba, ambapo baada ya kuwakabidhi chumba namba tisa, walikaa kidogo na baadaye walitoka nje kwenda kuoga na kuingia tena chumbani. “Ilipofika asubuhi ya saa nne muda wa wapa
Half the schools in Musoma lack toilets`
- Get link
- X
- Other Apps
`Half the schools in Musoma lack toilets` More than half of primary and secondary schools in Musoma District, Mara Region have no toilets, the situation which is said to contribute to persistent cholera outbreaks. Musoma District Planning Officer Yaled Mgula revealed this when presenting budget proposals for the year 2010/11 in the district’s full council meeting held on Friday. He said sometimes the students and teachers were forced to cut short sessions so that they can go back home or in the surrounding bushes to respond to short and long calls. Mgula said plans were underway to close the schools to avoid cholera outbreaks during the rainy season. Meanwhile, Mgula said that apart from toilets, the schools also face an acute shortage of teachers’ houses. However, he said the government was working hard to address the problem. In another development, Musoma Rural District Council is planning to purchase a speed boat to be used by fisheries officers to intensify patrols on Lake Victor
Poland yaomboleza kifo cha Rais Kaczynski
- Get link
- X
- Other Apps
Poland imetangaza siku saba za maombolezi kufuatia kifo cha Rais Lech Kaczynsk maafisa wengine waandamizi wa serikali katika ajali ya ndege, magharibi mwa Urusi. Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk, alisema hili ni janga kubwa kuwahi kutokea nchini humo katika historia ya siku za hivi karibuni. Maelfu ya watu, wengi wao wakitokwa na machozi, waliizingira ikulu katika mji mkuu,Warsaw, wakiweka mashada ya maua na mishumaa. Waziri Mkuu wa Urusi, Vladimir Putin, amesema atasimamia uchunguzi kuhusu ajali hiyo ya ndege, karibu na mji wa Smolensk, ambapo miongoni mwa waliouwawa ni mke wa Rais Kaczynski, na viongozi wengine kadhaa waandamizi wa kijeshi na wa kiraia kutoka Poland. Bw Putin alizuru eneo la ajali akiambatana na Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk. Waongozaji wa safari za ndege wa Urusi walisema rubani wa ndege hiyo alijaribu kutua wakati kukiwa na ukungu mkubwa, akipuuza ushauri aliopatiwa wa kuielekeza ndege hiyo kwingineko kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa. Ujumbe wa Poland uli
- Get link
- X
- Other Apps
Rapa matawi ya juu wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Emmanuel Kalonji ‘Toto Ze Bingwa’, anasakwa na Vijana wa Mwema (Polisi) kwa tuhuma za kumshushia kipigo Rapa mwenzake, Kanal Top na kumvunja mkono. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Adventure Mjini Moshi wakati Bendi hiyo ilipokuwa huko kwa ajili ya shoo ya Mkesha wa Pasaka. Chanzo chetu cha kuaminika kililitonya Ijumaa kuwa, awali Kanal Top alionekana akipanda stejini kufanya makamuzi kabla ya kushuka chini kumpisha rapa mwenzake Toto Ze Bingwa kuendeleza libeneke ambapo naye baadaye alishuka na kumpisha Kanal Top tena. Ikadaiwa kwamba, wawili hao waliendelea na kupishana kwa staili ya ‘anza wewe, nitafuata’, lakini mwishowe Kanal Top alimalizia kuchana mistari kisha kushuka chini. Ikazidi kudaiwa kuwa, wakati Kanal akishuka chini alipokelewa na rafiki yake mmoja wa huko Arusha na kuanza kupiga naye stori ambapo ghafla alitokea Toto Ze Bingwa na kuanza kumchimba mkwara kuwa atamfanyia kitu mbaya. “Jam
LIYUMBA AFUTIWA SHITAKA NA MAHAKAMA!!
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka mawili, kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221 leo ameondolewa shitaka la kutumia vibaya madaraka na hivyo kubaki na kosa moja.Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alifutiwa shitaka hilo baada ya mawakili wa upande wa utetezi kutoa vielelezo vilivyothibitisha kuwa mteja wao hakuwa na kesi ya kujibu.Mshitakiwa huyo amerudishwa Keko mpaka Aprili 22 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.kwa hisani ya http://www.globalpublisherstz.com/ na www.fullshangwe.blogspot.com
KARIBU SANA MWANA BLOGGER ULINGONI
- Get link
- X
- Other Apps
Huyu ni Augustino anayepatikana pale Musoma "Radio Victoria" kama Radio Presenter soon atafungua blog yake mpya itakayokuwa inajulikana kwa link ya www.mwanawaafrica.blogspot.com sooo utapata info kibao za kitaa,kimataifa,so once itakapokuwa tayari raia mtapewa info,itakuwa kiutofauti zaidi na blog nyingine kwa mwonekano wake.Be ready for that wadau.....