MWANAFUNZI WA KIKE AUWAWA KIKATILI GESTI
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Sara Nguzo, aliyekuwa akiishi Kigogo Mbuyuni, Dar es Salaam, amekutwa ameuawa chumba namba 9 cha nyumba ya kulala wageni iitwayo Makambe, iliyopo Ilala Mchikichini jijini.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia Aprili 5, mwaka huu ambapo uchunguzi wetu unaonesha
Mwanafunzi huyo alifika katika gesti hiyo na kijana mmoja na kuchukua chumba kwaajili ya kujipumzisha.
Wandishi wetu walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kumhoji mhudumu aliyejitambulisha kwa jina la Pricila Shirima, ambaye ndiye aliyewapa chumba alisema;
“Mwanafunzi huyo alifika kwenye gesti hiyo na mwanaume ‘Fataki’ mmoja mrefu, mweusi aliyevaa kofia nyeusi na kaptula, majira ya saa mbili usiku.
“Walipofika waliomba niwapatie chumba, ambapo baada ya kuwakabidhi chumba namba tisa, walikaa kidogo na baadaye walitoka nje kwenda kuoga na kuingia tena chumbani.
“Ilipofika asubuhi ya saa nne muda wa wapangaji kurudisha vyumba au kuongeza mkataba wa kuendelea kupanga, niliwagongea kwa muda mrefu lakini hakukuwa na dalili za mtu kufungua mlango.
“Hali hiyo ilinipa wasiwasi kwamba huenda kulikuwa na tatizo hivyo, nilipiga simu kuwaita Polisi, ili kuja kuangalia kama kuna tatizo limetokea chumbani humo.
“Polisi walipofika walivunja mlango wa chumba hicho na kumkuta binti huyo ameshafariki dunia akiwa uchi na shingo yake ikiwa na michubuko, wakauchukua mwili wake na kwenda kuuhifadhi Hospitali ya Amana kwa uchunguzi na mimi kunipeleka polisi Pangani kwa mahojiano,” alisema Mhudumu huyo.
Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejimbulisha kwa jina la Salum Nguzo, alisema siku ya tukio alikuwa mkoani Morogoro kikazi na alipigiwa simu kuwa binti yake amepotea.
Nguzo alisema baada ya muda alipigiwa simu na mkewe na kupewa taarifa kuwa mwili wa binti yao umepatikana akiwa amefia gesti na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Amana jijini.
“Tulienda Hospitali ya Amana na kuutambua kuwa ni mwili wa binti yangu, hivyo ilibidi tupange shunguli za mazishi ambapo tuliusafirisha kwenda Kijiji cha Kerenge mkoani Tanga kwa mazishi,” alisema Nguzo.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka muuaji wa mwanafunzi huyo ambaye mpaka sasa bado hajafahamika!
habari hii ni kwa hisani ya blog ya www.umbeabongo.blogspot.com
Comments
Post a Comment