BUNGE KUJADILI HOJA YA KUMN'GOA ZUMA JUMANNE

Bunge kujadili hoja ya kumn'goa Zuma Jumanne
Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.
Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka yake.
Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma
Vyama vya upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa makazi yake licha ya kushauriwa asifanye hivyo.
Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati nyumba yake ya binafsi.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kimekuwa kikimshinikiza ajiuzulu
Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atatakikana kuzirejesha.
Rais Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya kikatiba uliompata na hatia na akaapa kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama ilivyoamua mahakama.

Chanzo: BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA