RC Magesa Mulongo aagiza kuondolewa Mganga wa zahanati na kuhojiwa Mhandisi wa maji Wilaya


Hapa Mulongo akiwa zahanati ya Surubu
MKUU wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,ametoa maagizo ya kuondolewa mara moja mganga wa zahanati ya Surubu iliyopo Kata ya Manga wilayani Tarime na kulitaka jeshi la polisi kumuhoji mhandisi wa maji wa wilaya kwa ubovu wa mradi.

Maagizo hayo ameyatoa ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara ya siku 15 kuzungukia wilaya na halimashauri zote za mkoa wa huo ikiwa na lengo la kuangalia shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa.

Akiwa katika Kijiji cha Surubu kwenye zahanati ya Kijiji hicho,Mulongo alikutana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya mganga wa zahanati hiyo,Julius Nyakitamuri,aliyelalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Alisema kutokana na malalamiko yaliyotolewa na wananchi na kwa kutoa ushahidi wa kuitwa kusaidia mama mjazito kujifungua na kushindwa kufika na kupelekea kujifungulia nje ya zahanati inaonekana namna anavyoshindwa kusaidia jamii hivyo hana sababu za kuendelea kuwepo.

"Mganga wa wilaya naomba ukakae na huyu mtu ofisini kwako na otaona na namna ya kufanya na baada ya siku mbili naomba utafute mganga mwingine umlete kwenye zahanati hii ili wananchi waendelee kupata huduma za afya.

"Tumeshaweka utaratibu mtu akiharibu sehemu moja hawezi kupelekwa sehemu nyingine hivyo utaenda nae ofisini kwako na utajua cha kufanya maana hatuwezi kuwavumilia watu wa namna hii wakati wananchi wanaendelea kuumia,"alisema Mulongo.

Akiwa kwenye Kijiji cha Gibaso,Kata ya Kwihancha,mkuu huyo wa mkoa alimuagiza kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,kumchukua mhandisi mshauri wa maji wa wilaya ya Tarime,Vita Mkupa,kutoa maelezo juu ya mradi wa maji uligharimu milioni 318 na maji kushindwa kutoka.

Alisema licha ya kuchukuliwa kwa mhandisi huyo lakini pia mchimbaji wa kisima cha mradi huo kampuni ya Maswi Drilling na mtaalamu mshauri wa mradi, kampuni ya Net'was Tanzania,ili kutoa maelezo ya kina juu ya mradi huo kutokana na kulipwa fedha zote wakati huduma ya maji haipo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema jeshi la polisi lihakikishe linawapata wahusika wote wa mradi huo na kutoa maelezo ya kutosha kwa kuwa serikali ilitoa fedha za mradi ili wananchi wapate huduma ya maji na badala yake wananchi wameendelea kulalamikia ukosefu wa maji.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Magesa Mulongo akiangalia shimo la choo lililoachwa tangu mwaka 2013 kwa ajili ya choo cha walimu wa shule ya msingi Manga iliyopo wilayani Tarime na kutoa maagizo kijengwe mara moja

Waziri Mulongo akizungumza na wananchi wanaopata huduma kwenye zahanati hiyo huku kushoto akiwepo mganga aliyeondolewa kwenye zahanati hiyo

Mganga wa zahanati aliyeondolewa na mkuu wa mkoa

Moja ya vyanzo vya maji alivyotembelea mkuu wa mkoa

Mkuu wa mkoa akipanda kwenda kuangalia bwawa

Hapa akisikiliza maelezo

Mulongo akimsikiliza mhandisi wa maji wa wilaya ya Tarime (aliyenyoosha kidole) ambaye alikabidhiwa kwa jeshi la polisi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA