Taarifa ya Ofisi ya Bunge ya mabadiliko ya kusikia na kuonesha vikao vya bunge

TAARIFA KWA UMMA

MABADILIKO YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA RADIO NA

TELEVISHENI WAKATI WA VIKAO VYA BUNGE
___________

1.0. UTANGULIZI

Ili kuhakikisha kuwa Matangazo ya Bunge yanaendelea kurushwa na Televisheni nyingi hapa Nchini. Ofisi ya Bunge imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano ujao wa Bunge la Bajeti unaoanza tarehe 19 Aprili, 2016. 

Huu ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio yake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao.

Jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

2.0 UTARATIBU MPYA WA URUSHAJI MATANGAZO

Ili kuhakikisha kuwa vituo vya Redio na Televisheni vinapata matangazo ya Bunge, kila kituo cha Televisheni na Redio kitatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa yafuatayo:

3.0 HITIMISHO

Mabadiliko haya hayataathiri usajili wa Waandishi wa Habari wengine kuja Bungeni kwa ajili ya kufanya Coverage ya Shughuli za Bunge ambazo hazihusishi kuingiza kamera ndani ya ukumbi wa Bunge. Utaratibu huu mpya, utakuwa umesaidia kuondoa hali ya kila Kituo cha Televisheni kufunga Mfumo wake wa Kurusha Matangazo kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma na badalayake yatapokelewa katika Vituo vya Televisheni na Redio kupitia Masafa tajwa hapo juu. Utaratibu huu ni wa kawaida katika

Mabunge takribani yote Duniani husani wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM.

15 Aprili, 2016.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA