Mkakati wa RC wa Dar kuhusu ombaomba, muziki baa na majengo yasiyo na maegesho


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi, amejipanga kuanza na mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru wamiliki wa baa kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.
  • Makonda ametoa siku sita (kuanzia leo mpaka Aprili 18) kwa ombaomba ndani ya jiji la Dar es Salaam wawe wameondoka.
  • Pia Makonda amesema wamiliki wa baa wanaowapigia watu kelele, wafuate sheria walizopewa. 
Kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.
Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake, ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini atakayoilipa mtuhumiwa mwenyewe. 
  • Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari (parking) walipe faini na kuweka utaratibu wa kuegedha wapi magari yao au kubomoa majengo yao.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA