JIPU LINGINE KUTOKA IRINGA

Taarifa kutoka kwa  Comrade,Goliath Mfalamagoha,kwa taarifa hii,haya ndiyo masuala ambayo wabunge wetu mnatakiwa mkayajadili huko bungeni.

Kiwanda cha karatasi kilichopo wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kiitwacho Mufindi paper mills LTD (MPM) zamani Southern Paper Mills (SPM) kilichokuwa kinamilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Tanzania 100%, chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Kwasasa kinamilikiwa na kampuni ya RAI GROUP LIMITED ya nchini Kenya.

Kiwanda hiki cha mgololo kilianzishwa rasmi na kuzinduliwa na Rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, hayati Mwl. JULIUS. K. NYERERE mwaka 1985 kikiwa na thamani ya Bilioni HAMSINI za Kitanzania kwa wakati huo, jukumu lake kuu ilikuwa kuzalisha karatasi kwa kutumia malighafi za ndani toka katika msitu wa Saohili Mafinga, lengo ilikuwa ni kufanya biashara na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Tarehe 24/01/1997 kwa waraka wa serikali (Government Notes) namba 33, Serikali ili-specify Kiwanda na kukiweka chini ya tume ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC) iliyopewa jukumu la kusimamia shughuri za Kiwanda zikiwemo huduma kwa wafanyakazi wanaotunza kiwanda kwa kufanya uzalishaji mdogo mdogo (mill warming) na pia kutafuta mwekezaji (kukinadi hatimaye kukiuza kiwanda).

Tarehe 13/02/2004 kiwanda kilikabidhiwa rasmi kwa Rai Group ya Kenya kwa maelezo ya kuwa wao ndio wanunuzi wa Kiwanda hicho adimu barani Afrika, hakuna taarifa rasmi za bei ya ununuzi wa kiwanda hicho lakini inatajwa kuwa kiliuzwa kwa Shilingi bilioni MOJA za Kitanzania.

Leo hii kiwanda hakizalishi karatasi tena, mitambo imeng'olewa na kuhamishiwa kenya, ambapo pale Mgololo zinazalishwa malighafi tu za karatasi, kisha husafirishwa Kenya, nakutengenezwa karatasi kisha hurudishwa nchini kutuuzia Karatasi hizo,

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA