MTAZAMO NA USHAURI KUTOKA KWA COMRADE MALISA KWENDA KWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

MFIKISHIENI JPM..
By Malisa GJ,


Kwa moyo wa dhati kbs nampongeza Rais Magufuli ktk jitihada zake za kubana matumizi. Lakini nina mambo mawili ya kumshauri;
‪#‎MOSI‬;
Kubana matumizi bila kubuni vyanzo vipya vya mapato ni kazi bure. Kama atawanyima madereva safari za Dodoma, akapunguza posho za watumishi Lakini bado tukaendelea kupewa 04% kwenye madini na 09% kwenye gesi ni kazi bure.
Kama atapunguza mishahara ya watumishi, atazuia safari za nje, ataondoa sijui semina na warsha serikalini lakini akafumbia macho "mbio za mwenge" naona ni kazi bure pia.
Namshauri badala ya kulazimisha malaika waishi kama mashetani, ni vizuri ajitahidi kuwafanya hao mashetani (watanzania maskini) waishi kama malaika. Falsafa ya kufanana si kumfilisi tajiri ili awe maskini kama wewe, bali kumsaidia maskini apande na kufanana na tajiri.
Kama kipato hakitoshi kwenye familia dawa sio kubana matumizi na kulazimisha watoto wale dagaa kila siku, dawa ni kuwajibika zaidi na kutafuta njia mbadala ya kukuza kipato ili watoto waweze kubadilisha mboga.
‪#‎PILI‬;
Napenda kumuuliza JPM anapata wapi ujasiri wa kuwakemea watumishi wenye mishahara miwili (au zaidi) wakati mawaziri wake wote wana mishahara miwili? Mawaziri wote wana mshahara wa uwaziri na wa ubunge. Wana posho za uwaziri na za ubunge. Wengine ni wajumbe wa bodi za taasisi mbalimbali huko nako wana posho. Bado posho za kamati za bunge.!
Waziri ana "shangingi" la uwaziri, ana "shangingi" la Ubunge. Ana hela ya mafuta ya ubunge (lita 1000 kila mwezi kwa wabunge wa majimbo), ana hela ya mafuta kama Waziri. Mawaziri ni majipu makubwa zaidi kuliko hao watumishi wenye mishahara miwili.
Nashauri anza na mawaziri kwanza. Wapokee mshahara mmoja tu, posho moja tu, gari moja tu. Asiyetaka ajiuzulu.
Rasimu ya Warioba ilizuia Waziri kuwa Mbunge. Lengo lilikua kupunguza mgongano wa kimaslahi kati ya bunge na serikali, lakini pia kuwaondolea Mawaziri mishahara na posho mbilimbili. Lakini CCM kusikia posho mbilimbili na mishahara miwili-miwili inafutwa wakaitupilia mbali rasimu ya Warioba.
Sasa Mheshimiwa Rais umeacha kuwaona hao unakuja kuhangaika na Mwalimu wa shule ya msingi Vigwaza darasa la 3B anayepokea mishahara miwili ambayo jumla yake haifiki hata posho ya waziri kwa siku moja? U cant be serious brother.
Anza na Mwenge, then futa mikataba yote ya kinyonyaji kama mikataba ya madini na gesi, then pandisha mishahara kwa watumishi wa umma, kisha punguza kiwango cha PAYE kwny mishahara, kisha boresha mazingira ya kazi kwa watumishi, halafu rudisha upya bunge la Katiba na rasimu ya Warioba, ndo uje kwenye mishahara miwili. Na ukifika hapa anza na mawaziri.
Mawaziri wako ndio mabingwa wa kupokea mishahara miwili. Wabane wao kwanza ili waliopo chini washtuke na kuchukua hatua.
Lakini kukimbizana na watumishi wanaojilipa mishahara miwili wakati mawaziri wako wote wana mishahara miwili itz worthless. Ni sawa na kumshangaa mtoto wa jirani yako kunywa "Castle lite" wakati mwanao kalowea kwenye "viroba" na "chang'aa".!!
@MALISA GJ.!

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA