WAKURUGENZI WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) WATUMBULIWA MAJIPU


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi watendaji wakuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya kupisha uchunguzi kuhusu wizi na udanganyifu uliofanywa katika akaunti ya madai ya NHIF mkoa wa Mara.

Taarifa za awali zinaonesha zaidi ya shilingi bilioni 2.9 zimeibwa kwa njia ya udanganyifu kutoka katika akaunti yamadai ya NHIF mkoa wa Mara ambazo zimekuwa zikichukuliwa kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka mitatu tangu 2013.

Waliosimamishwa ni kaimu mkurugenzi mkuu Michael Mhando, mkurugenzi wa fedha na vitega uchumi Deusdedit Rutazaa, mkurugenzi wa mifumo habari Ally Othman na mkaguzi mkuu wa ndani Anne Maneno.

Waziri Ummy Mwalimu pia ameagiza mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali kufanya uchunguzi maalum wa mfumo mzima wa utoaji madai wa NHIF pamoja na akaunti zake katika mikoa yote ili kubaini ukubwa wa tatizo na hatua kuchukuliwa.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA