Posts

Showing posts from August, 2014

MAPYA KUTOKA BRAZIL,KUNA MJI UMEJAA WANAWAKE WAREMBO WANAOTAFUTA WANAUME MAKAPERA

Image
Mji mmoja nchini Brazil ambao una wanawake watupu, wengi wakiwa vijana na "warembo mno" umetoa wito wa kutaka vijana wa kiume - ambao bado ni makapera (yaani single). Kwa mujibu wa tovuti ya Metro, mji huo uitwao Noiva do Cordeiro, una watu 600, ambao wote ni wanawake. Watoto wa kiume wanaozaliwa katika mji huo hutakiwa kuondoka wakitimiza umri wa miaka 18, na waume kadhaa wenye wake zao huko, hutakiwa kwenda mjini humo si ku za wikendi tu. Wanawake vijana katika mji huo sasa wamechoshwa na kutokuwepo na wanaume na wametoa wito kwa wanaume makapera kujitokeza. "Hapa, wanaume pekee tunaokutana nao, ama wameoa, au ni ndugu zetu, kila anaye kuja hapa ni binamu. Sijapata kubusu mwanaume kwa muda mrefu," amesema Nelma Fernandes, 23, akizungumza na gazeti la Mirror. "Sote tunaiota siku ambayo tutakutana na mwanaume na kupendana naye na kufunga ndoa. Lakini tunapenda kuishi hapa, na hatutaki kuuhama mji wetu kwenda kutafuta waume....

SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR NA VIUNGA VYAKE KWA BURUDANI KALIII ILIYOKWENDA SHULE

Image
Diva wa Skylight Band Mary Lukos Akiimba kwa uzuri kabisa Ndani ya kiota cha burudani Thai Village.Bendi yako machachari na inayopendwa zaidi ndani ya Jiji la Dar es salaam na viunga vyake vyote Skylight Band inakukaribisha wewe mdau,mpenzi na shabiki wa kweli Leo hii kuanzia mida ya Tatu kamili ndani ya ukumbi wa Thai Village masaki,ambapo burudani ya nguvu itaporomoshwa na wanamuziki mahiri wa bendi hiyo kama Aneth Kushaba,Mary Lukos,Digna Mpera,Sam Machozi,Donode,Joniko Flower na Sony Masamba.Njoo upate muziki mzuriiiii na ladha zote za kiafrika na ulaya pamoja na suprizeee kibaooooo. Digna Mpera akiimba na kucheza kwa umahiri kabisa ili kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wake Anaitwa Aneth Kushaba A.K.A AK47 au Le Meneja Her Self akiimba kwa mikogooo safi ndani ya Thai Village ili kuwapa burudani ya nguvu Mashabiki wake Le Meneja Her Self  Akiimba kwa Hisia Kaliiiiii Kabisaaaaa Aneth Kushaba(katikati)akiongoza madiva wenzake wa Skylight Band Digna Mpera(kulia) n...

"BUNGE LAJIGEUZA TUME YA JAJI WARIOBA NA HABARI" ZINGINE ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE, AGOSTI 26 YAPO HAPA

Image