SHINDANO LA KUMWAGIWA MAJI YA BARIDI KWA WATU MAARUFU LAVUTIA INSTAGRAM


Shindano linalowahusisha watu maarufu la kumwagiwa maji ya baridi yenye barafu yakiwa katika ndoo (celebrities ice bucket challenge) linaweza kuwashangaza watu wengi kwa jinsi linavyofanyika, kama umekuwa mfatiliaji mzuri wa instagram na kuwafollow wanamuziki maarufu nchini marekani wamepost video wakimwagiwa maji, baadhi ya ma star hao waliopost video hizo ni Chris Brown, J Lo, The Game, Snoop Lion, Ludacris na Justin Bieber.

Shindano ili lina lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa wa  uti wa mgogo  unaojulikana kama  “ motor neuron disease” ambapo katika uti wa mgongo kuna vichocheo vya aina mbili ambavyo ni sensory na motor neurons ambazo usafirisha taarifa kwenda kwenye ubongo. Shindano ili pia linabeba ujumbe wa kuwafahamisha watu duniani juu ya uwepo wa ugonjwa huu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA