Mtuhumiwa azua kihoja mahakamani Rwanda


Rwanda imekuwa ikiendedesha harakati za upatanishi na pia kuwakumbuka waliokufa katika mauaji hayo
Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Emmanuel Mbarushimana amekataa uendeshwaji wa kesi yake na mahakama ya Kigali kwa kutoa pingamizi kwamba hana haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.
Mshukiwa huyo alikabidhiwa Rwanda na nchi ya Denmark mapema mwezi wa saba mwaka huu ili kujibu mashitaka ya kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Mushukiwa huyo Bwana Emmanuel Mbarushimana amesema kesi yake haiwezi kusikizwa hadi pale atakapopata haki zilizo sawa na mwendesha mashitaka.
Hoja yake ilikuwa kwamba ni lazima na yeye aruhusiwe kukaa badala ya kusimama wakati kesi yake ikisikilizwa na wakati huo huo mwendesha mashitaka asimame badala ya kukaa kama ilivyozoeleka.
Aidha, amesema kuwa hajafurahia utaratibu unaotumiwa wa kuingia katika chumba cha mahakama ambapo mwendesha mashitaka na majaji wanaingia kwa kutumia mlango mmoja kinyume na mushitakiwa.
Mwendesha mashitaka amemshitaki kwa kushiriki katika mauaji dhidi ya watutsi yaliyotokea katika maeneo mbali mbali katika mkoa wa zamani wa Butare kusini mwa Rwanda.
Mushukiwa pia ameleta hoja nyingine ya kwamba hana wakili.
Swala hilo la kuwa na wakili lilikuwa limeshajadiliwa katika kikao cha kesi kilichotangulia ambapo alipewa muda wa kuchagua wakili anayetaka.
Wakati huo alipewa orodha ya mawakili 500 miongoni mwa mawakili wanaohudumu hapa nchini na kuikataa.
Alipendekeza kupewa orordha nzima ya mawakili wote kwa ujumla ili amchague mmoja anayetaka.Kipindi alichokuwa amepewa kuchagua wakili huyo kilikuwa kimemalizika.
Mahakama imesema kuwa hoja hizo haziwezi kuzuiya kesi hasa ikiwa ni kesi ya kukiri ama kukana mashtaka dhidi yake;jambo alilokataa kata kata akisema mahakama haina uhuru wala haki.
Imetangazwa kuwa Uamuzi kuhusu mabishano hayo utatolewa kesho.
Emanuel Mbarushimana mwenye umri wa miaka 50 alikabidhiwa Rwanda na mahakama ya Denmark mapema mwezi uliopita ili kujibu tuhuma za kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

chanzo:bbc swahili

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA