#TeamWema WAPEWA MAKAVU BAADA YA KUMDISI DIAMOND PLATNUMZ

Baada ya mashabiki wa mwanadada Wema kumjia juu mwanamuziki Diamond Platnumz kuhusu tuhuma za yeye kumtumia mwanadada huyu kimwili zaidi bila kumuendeleza, hatimaye rais huyu wa kundi la WCB ameamua na yeye kufunguka haya mazito juu ya kauli hizo. Kupitia ukurasa wake,
Na hiki ndicho Diamond alichokiandika
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu... kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe...
Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng'ombe wake Kwenye Maji safi....ila yeye ng'ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!... leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!....Mxieeeeeeeew!

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA