MTOTO WA RAIS KIZIMBANI KWA UFISADI


Karim Wade

Kesi ya ufisadi dhidi ya Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade imeanza kusikilizwa huko Dakar Senegal. Hata hivyo kesi hiyo inaanza kusikilizwa mshitakiwa akiwa kizuizini katika gereza kuu la Dakar, Rebeuss kwa mwaka mmoja sasa.
Waziri huyo wa zamani atatakiwa kuieleza mahakama vyanzo vya utajiri wake wa Uero milioni 178.

Hata hivyo kiwango hicho cha fedha kinadaiwa kuwa kidogo ikilinganishwa kile kilichosababisha kukamatwa kwake ambacho ni Euro bilioni moja.
Seydou Diagne, mmoja wa wanasheria wa Karim Wade, amelalamikia mashitaka hayo na kuyaita ya kisiasa akidai kuwa kitu pekee kinachowasukuma wanao mshitaki mteja wake.
Wanasheria wake pia wamedai hata hiyo mahakama itakayotumika kuchunguza matumizi mabaya ya ofisi haina uwezo wa kuisimamia kesi hiyo.
Hii ni moja ya kesi za kuwatafuta vigogo waliozitumia vibaya ofisi zao wakati wa utawala wa Rais Abdoulaye Wade.

chanzo: BBC swahili.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA