UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA.

Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda

Nchi ya Uganda ambayo ilidiriki kusimama kidete kupinga mapenzi ya jinsia moja hatimaye wameifuta sheria dhidi ya ushoga, ni maswali mengi watu watajiuliza je ni kwa sababu ya vikwazo vya nchi za Magharibi ambavyo viliwekwa baada ya Uganda kupitisha mswada huo na kuwa sheria. Mwandishi wa BBC anaelezea hali ilivyokuwa mpaka kufuta sheria hiyo.

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.

Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika kuingilia kati. 

Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.
Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia moja.

Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa. 

chanzo bbc swahili

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA