MPAKA SASA HAKUNA WAGONJWA WALIOBAINIKA KUWA NA EBOLA TANZANIA, VIPIMO VYADHIBITISHA.

Jana zimeibuka habari kwamba kuna wagonjwa wawili ambao wameonekana kuwa na dalili za Ebola, ambao ni wageni waliokuwa wakiingia nchini  wakitokea nchi ya Benin kupitia account ya Dr. Isaac Maro ambaye ni daktari pia ni mtangazaji wa kituo cha radio Clouds fm ya jijini Dar Es salaama, amedhibitisha kwamba wagonjwa wale walikuwa na magonjwa mengine lakini sio Ebola kama taarifa za mwanzo zilivyo sambaa.

Post by Isaac Maro.

By Isaac Maro
"Ripoti inayosambaa kuwa kuna wagonjwa Wawili wamepelekwa hospitali ya Temeke wakihisiwa kuwa Na Ebola ni kweli sema Baada ya Vipimo kufanyika Na historia kuchukuliwa imeonekana wote wana Maradhi mengine ya Siku nyingi Na sio EBOLA! Narudia tena Hakuna Maradhi ya Ebola Tanzania Mpaka Sasa...sema shukrani KWA wote waliopambana kuhakikisha wagonjwa wanapelekwa KWA Ajili ya Vipimo! HIVI ndio tunatakiwa kufanya....ukiona mtu Ana Dalili Za Maradhi hakikisha unapaza sauti! God bless Tanzania".

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA