Burundi: watu zaidi ya 5 kutoka familia moja wachomwa moto
Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016.
Watu
wasiopungua watano kutoka familia moja wameuawa kwa kuchomwa moto wakiwa
hai katika kijiji cha Bucana, Wilayani Gitobe, mkoani Kirundo,
kaskazini mwa Burundi.
Kwa
mujibu wa Mshauri wa Mkuu wa wilaya Gitobe, wahanga kabla ya kuchomwa
moto na kuteketea ndani ya nyumba yao, walichomwa visu.
Afisa
huyo ameongeza kwamba idadi ya watu walioteketea kwa moto inaweza kuwa
kubwa zaidi: "inasadikiwa kuwa kuna watoto ambao walikua ndani ya nyumba
hiyo, ambao hawakupatikana, kutokana na moto mkali ambao ulikua
ukiwaka, " amesema Mshauri wa Mkuu wa Wilaya ya Gitobe.
Visa vya
mauaji vimekithiri katika nchi hiyo ndogo ya Afrika ya Kati. Burundi ni
nchi ya Ukanda wa Maziwa Makuu ambayo imeathirika na mauaji, hasa baada
ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja, baada
ya kuuawa kwa rais wa kwanza kutoka kabila la Wahutu, Melchior Ndadaye
aliyechaguliwa mwaka 1993 kuliongoza taifa hilo, ambalo kwa miaka zaidi
ya 60 lilikua likiongozwa na kabila moja tu ya Watutsi.
Mashirika
yanayotetea haki za binadamu yanabaini kwamba watu zaidi ya 270,000
wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani na
Ulaya kwa kuhofia maisha yao, na wengine waliosalia nchini humo
wameendelea kushuhudia visa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauaji,
uporaji, unyanyasaji, ... Mashrika hayo yameendelea kuishtumu serikali
kuhusika na visa vyote hivyo vinavyoendelea kushuhudiwa nchini humo.
Comments
Post a Comment