NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYENYE SAINI
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami akiwaeleza waandishi wa
habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho
vipya vyenye saini ya mwenye kitambulisho. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Uzalishaji Vitambulisho Bw. Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis.
Kaimu
Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis akifafanua kwa
waandishi wa habari kuhusu faida za vitambulisho vya taifa jana jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Bw.
Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Bi. Rose Mdami.
Baadhi ya
waandishi wa habari wakiangalia video ya faida za vitambulisho vya
Taifa iliyoandaliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa
ajili ya kuelimisha umma kwenye mkutano wa Mamlaka hiyo na waandishi wa
habari uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na Fatma Salum (MAELEZO)
Frank Mvungi-Maelezo
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa
vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa
Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jana jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Mdami alisema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania
wote wanapata vitambulisho vya Taifa ambapo katika hatua ya kwanza
mamlaka hiyo inachakata taarifa za wananchi walizotoa wakati wa
kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana.
Utoaji wa
vitambulisho hivi vyenye saini ya mwombaji utasaidia kuwatambua
wahusika pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii.
“Upatikanaji
wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la
Watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine
inayosimamia utumishi wa umma” alisisitizaMdami.
Utoaji
huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za utambulisho kwa wananchi
ilizisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati mchakato wa
kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.
Mdami
alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili ya uhakiki
wa taarifa hizo.
Comments
Post a Comment