MATUKIO YA UBAKAJI WA WATOTO YAFIKIA 2358 KWA MWAKA
Jonas Kamaleki-Maelezo- Dodoma
MATUKIO
ya ubakaji watoto yameongezeka hadi kufikia 2358 kwa mwaka 2015
ikilinganishwa na 422 ya mwaka 2014 na kufanya vitendo hivyo kuwa tishio
kwa watoto nchini.
Hayo
yalibainishwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu kwenye mkutano na waandishi
wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
“Asilimia
49 ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto hufanyika majumbani,
wakati asilimia 23 hufanyika njiani wakati wa kwenda au kutoka shule na
asilimia 15 hufanyika shuleni,”alisema Ummy.
Akionyesha
kusikitishwa na ongezeko hilo la vitendo viovu dhidi yawatoto, Ummy
alisema kuwa hali hii inatisha na kukera kwani ndani ya miezi mitatu
mwaka huu yaani januari hadi Machi 2016 matukio 1765 yameripotiwa katika
vituo mbalimbali vya polisi.
Aidha,
Ummy alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa
Mataifali linaloshughulikia masuala ya watoto (UNICEF) ilifanya utafiti
kuangalia hali halisi ya Ukatili dhidi yawatoto na kubaini kuwa
wasichana 3 kati 10 na mvulana mmoja kati ya 7, wamefanyiwa ukatili wa
kingono angalau mara kabla ya kutimiza miaka 18.
Kwa
mujibu wa Wazirti Ummy alisema Utafiti huo pia umeonyesha kuwa wasichana
4 kati ya 10 na wavulana 3 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili zaidi ya mara
tatu kabla ya kufikisha miaka 18, na wasichana 6 kati ya 10 wamefanyiwa
ukatili ndani ya familia zao na msichana mmoja hadi wawili wamefanyiwa
na walimu wao.
“Msikubali
kuwalaza chumba kimoja watoto wa kike na ndugu wa kiume kwani tabia
hizo chafu zimekuwa zikifanywa na watu wa familia,” alisema Ummy.
Aliongeza kuwa vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto vina athari kubwa sana katika ustawi wa watoto..
Aidha
alisema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kisera na
kisheria katika kusimamia utekelezaji wa haki ya motto ya kuishi,
kulindwa na kuendelezwa, ikiwemo na kufanya mabadiliko ya Sheria ya Ndoa
ya Mwaka 1971 inayohalalisha motto wa miaka 15 kuolewa kwa ridhaa ya
wazazi na wa miaka 14 kwa kibali cha mahakama,” alisema Ummy.
Alisisitiza
kuwa muswada wa Sheria ya Ndoa inabidi uletwe bungeni haraka
iwezekanavyo na kuongeza kuwa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria hiyo
yameshapelekwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Comments
Post a Comment