KUPANDA MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI DAR SASA NI KWA KADI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart),
David Mgwasa (kushoto),akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi
ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na
waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam
jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao
wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma
Rajabu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika
matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika
mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabar ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MRADI wa
Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma
kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo
iliyoanza rasmi jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji
wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili
kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa
muda mrefu kabla ya kuondoka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika
matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia
wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa
bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni
malipo ya mteja wao.
“Shilingi
4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda
eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara,
Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu” alisema
Rajabu
Aliongeza
kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha
abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na
changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
Alisema
licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaendelea kama
kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na huduma hiyo unatakiwa kupiga
*152*22#
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Comments
Post a Comment