WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO WA PILI WA MAENDELEO YA TAIFA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo. Anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mapango

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021 unalenga kuboresha maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha Sekta zinazoajiri watu wengi na walio masikini zinakuwa kwa kasi. 

Akizindua Mpango huo leo (Jumanne, Juni 7, 2016) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itahakikisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Uvuvi na Mifugo zinakua kwa kasi ya kuridhisha ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini. Amesema utekelezaji wa Mpango huo ambao umefungamanisha maendeleo ya viwanda na maendeleo ya watu na unatazamiwa kujibu changamoto ya umasikini Tanzania. 

Waziri Mkuu amesema katika Mpango huo kuna maeneo mbalimbali ya vipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango huo ni miradi mikubwa kama ya chuma cha Liganga, kufufua shirika la Ndege, Makaa ya Mawe Mchuchuma, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha standard Gauge ambayo matokeo yake yanatarajiwa kuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mingine. 

“Tunatarajia ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga nchi ambayo ina maisha bora, yenye amani, umoja na utawala bora, jamii inayojifunza na iliyoelimika, yenye uwezo wa kuzalisha na kuwa na ukuaji wa uchumi endelevu na wenye ushindani,” amesema. 

Waziri Mkuu Majaliwa amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ukuaji huo wa uchumi unakuwa shirikishi zaidi katika utekelezaji wa Mpango huu na kwamba uendelezaji wa viwanda ndio utakaoleta mafanikio makubwa karika mwelekeo huo. 

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema jumla ya viwanda 39 kati ya 106 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambavyo vilikuwa vya vinazalisha bidhaa za chuma, ngozi, korosho zana za kilimo, sabuni na mafuta ya kupikia wamevifunga na kutoviendeleza. 

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kwa Msajili wa Hazina itaendelea na zoezi la kuvirejesha viwanda hivyo Serikalini ili waangalie utaratibu mwingine ulio bora wa kuviendeleza kwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo. 

Amesema Mpango huo ambao utajikita zaidi katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na vile vilivyobinafsishwa ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi wengi. 

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ambao utahitimishwa Juni 30, 2016 Serikali ilifanikiwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara za lami na madaraja ya Kigamboni, Maligisu Nagoo, Mbutu na Ruhekei. Pia ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542), ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika maeneo ya Madimba na Songosongo, ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi vya Somanga-Fungu na Kinyerezi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati akizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kitabu cha mpango huo.

Mawaziri wakifurahi baada ya mpango huo kuzinduliwa.

Waziri Mkuu, Majaliwa akimkabidhi mpango huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson.

Waziri Mkuu, Majaliwa akimkabidhi mpsngo huo Mbunge wa Jimbo la Korogwe kwa niaba ya Kiongozi Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe ambaye ahakuwepo katika sherehe hiyo.

Waziri Mkuu, Majaliwa akiwa na viongozi wote waliokabidhiwa mpango huo.

Baadhi ya wazee na viongozi wa dini wakishiriki katika sherehe hizo

Philip Mpango akijadiliana jambo na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustino Mahiga akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.


Profesa Jumanne Maghembe na Balozi Mahiga wakifurahia jambo

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola akizungumza na Mahiga



Dk. Mpango akimkaribisha Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson

Naibu Spika akisalimiana na Mbuu wa Wilaya ya Dodoma mjini, Jasmine Tisekwa

Naibu Sika akizungumza na Nape pamoja na January Makamba

Waziri Mwijage akisalimiana na mmoja wa maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri Mkuu, Majaliwa akikaribishwa na Dk. Mpango

Waziri Mkuu Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Doroth Mwanyika

Baadhi ya wageni waalikwa

Dk. Mpango akiteta jambo na Waziri Mkuu Majaliwa

Kiongozi wa Dini ya Kiislamu akiomba dua ili mpango huo ufanikiwe

Kiongozi wa Dini ya Kikristo akiuombea mpango huo

Mawaziri wakiuombea mpango huo

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Majaliwa

Kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Wagogo cha Nyati kikitumbuiza










Majaliwa akiwa namawaziri

Waziri Mkuu, Majaliwa akiaga baada ya kuzindua mpango huo muhimu kwa Taifa
chanzo:mjengwablog.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA