OSCAR PISTRORIUS AKABILIWA NA KIFUNGO CHA MIAKA 15
Kusikiliza hukumu kwa mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius kuilianza Johannesburg jana. Mwanariadha huyo wa Olympic anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela baada ya mahakama ya rufaa kubadili adhabu ndogo na kumkuta na hatia ya mauaji.
Wanasaikologia wanasema, Oscar Pistorius ambaye alikuwa mashuhuri sasa ni mwanamume aliyevunjika, na anahitaji hospitali na sio jela.
Mwanariadhaa huyo alirejea tena kizimbani jana baada ya mahakama ya rufaa kumkuta na hatia ya mauwaji ya mchumba wake mwaka 2013. Saa anakabiliwa na kifungo cha takriban miaka 15. Kesi hiyo itaendelea hii leo mbele ya jaji Thokozile Masipa.
Daktari wa saikologia Jonathan Scholtz anasema matukio ya miaka michache ilopita yamemuathiri sana Pistorius.
Dkt Scholtz alisema kuwa, Pistorius ana viwango vya juu vya wasiwasi ambavyo ni vikubwa kwa viwango vya ki matibabu. Hii ni pamoja na dalili za kuwa na wasiwasi wa kujumuika na jamii na kadhalika. Kwa afya ya yake ya kiakili kiujumla, anaonekana amedhoofika tangu mwaka 2104. Mbali ya kuzorota kwa hali yake kiafya, anaonekana kuwa amekataa tamaa, na kuachia mustakbal wake mikononi mwa mwenyezi mungu. Yaani amevunjika. Na kwa maoni yangu kwa hali aliyonayo sasa, anahitaji kulazwa hospitalini.
Bila shaka ilikuwa miaka michache yenye mitihani.
Pistorius anasema mara kwa mara anakumbwa na hofu na wasiwasi. Anaendelea kusisitiza kuwa alidhani mchumba wake Reeva Steenkamp ni jambazi pale alipofyatulia risasi 4 kwenye mlango wa chooni uliokuwa umefungwa, na kupelekea kumuuwa mchumba wake, siku ya wapendanao mwaka 2013.
Waendesha mashtaka wanasema alikusudia kumuuwa Steenkamp pale alipofyatua risasi kwenye mlango wa choo nyumbani kwake Pretoria.
Kesi hio iliyochukua muda mrefu imefuatiliwa kwa karibu kote duniani, na ghadhabu ziliibuka pale jaji Masipa alipomhukumu mwaka 2014 kwa kuhusika na mauwaji, na kumpatia hukumu ya kifungo cha miaka 5 jela.
Aliachiliwa huru hapo October baada ya kutumika mwaka mmoja tu jela, na kisha hukumu yake ikapinduliwa na kubadilishwa na kukutwa na hatia ya mauwaji mwezi December.
Ni miaka mine tu ilopita pale Oscar Pistorius alikuwa akitambaa nakupendwa na umma kwa kuwa mlemavu wa kwanza kuweza kushindana katika mashindano ya Olympic
Hii leo Pistorius ni amedhoofu, mwembamba sana, amepinda kiasi na maisha yake yanaelezewa siyo kwa mafanikio yake, lakini maisha yake yanaelezewa kwa tukio baya lilitokea siku hiyo usiku
Comments
Post a Comment