WAZIRI NAPE NNAUYE AZINDUA STUDIO YA REDIO YA JAMII KATIKA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa
ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof.
Elifas Bisanda kwenda kuzindua Studio ndani ya Chuo hicho 27 Juni, 2016
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata
utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network
of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto)
akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira
Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania
(COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani
ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akijibu
baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua
rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani
ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akifafanua
jambo mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27
Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa
Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amezindua
studio ya redio ya jamii ya ‘Community Media Network of Tanzania’
(COMNET) katika Chuo kuku Huria( OUT ) itakayotumika kusambaza habari
maeneo yenye uhaba wa redio.
Uzinduzi
huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam,ambapo Mhe. Waziri amesema
kuwa studio hiyo itasaidia idadi kubwa ya wanachi wanaoishi vijijini
kupata habari kutoka Serikalini na kutoa mrejesho wa kile watakachosikia
kwa urahisi.
“Ni
Studio muhimu kwa ajili ya kusambaza demokrasia kwa watu hasa wale
waliopo vijijini kwa vile redio nyingi bado hazijawafikia”Alisema
Mhe.Nape.
Aidha
amewataka wanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa
umma katika chuo hicho kutumia studio hiyo kujifunza zaidi kwa
vitendo na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari
zenye ukweli kutoka vyanzo sahihi ili kutoa ujumbe wenye manufaa mazuri
kwa jamii.
Kwa
upande wake Makamu mkuu wa Chuo hicho Prof. Elifas Bisanda amesema
studio hiyo imeanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO) kwa lengo kutoa elimu kwa jamii
ambayo imekuwa haipati habari kwa urahisi.
Amewataka
wanahabari na wananchi kwa ujumla kufikisha habari katika studio hizo
kwa kuwa inatumia njia ya haraka na rahisi katika kufikisha ujumbe kwa
kushirikiana na redio mbalimbali za jamii.
Naye
mwakilishi kutoka Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia
Elimu,Sayansi,na Utamaduni(UNESCO) Bi. Zulimira Rodrigues amesema
studio ya redio ya ‘Community’ ipo kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii
kuhusu maendeleo ya wanawake na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Comments
Post a Comment